Monday, September 27, 2010

MTEMBEA BURE SI SAWA NA MKAA BURE

Leo nikiwa nafikiria nini nipost katika blogu hii nikagundua sina kitu kuanzia kichwani hata mtandaoni cha kuwashirikisha wasomaji wangu. Wakati najijifikirisha nilikuwa nasikiliza hiki kibao cha MUCHANA cha mchawi mwingine wa Kongo Kanda Bongomani. Nikaona niwashirikishe kuusikiliza kwa mara nyingine wimbo huu. Ila siwajui MAJINA YAO hao wadada wanaoitikia, wanaodakia na kucheza. Kuna anayewajua/wafahamu? Napenda sana muziki wa Kongo wa kuanzia 1996 kushuka chini. Huu wa siku hizi wa kia Fali Ipupa mbalimbali na mimi.




Kama unusikiliza sana muziki huu wa enzi za kabla ya 1996 utagundua kuna segment ya gitaa la solo kuachiwa litawale. Huwa nakipenda kifaa hiki hasa kikikunwa na anayekipatia kama Lokassa ya Mbongo hapo videoni.

Labels:

Wednesday, September 22, 2010

BARUA ENZI ZA MWALIMU



Naona kati ya huyu jamaa na huyu jamaa atakayetangulia kutuma barua hii atakubaliwa na Koero Mkundi

Labels: ,

Saturday, September 18, 2010

ANDIKA MAELEZO YA PICHA HII



Picha hii nimeitoa hapa. Leo tushindane kuandika caption (maelezo ya picha) za kubuni wenyewe. Atakayeandika caption ya kuvutia zaidi atakuwa mshindi wetu. Namna ya kumpata mshindi nitawaambia baadae.

Labels:

WEWE UNGEFANYEJE

Mwenyewe una dharura zako, huna hili wala lile na unahitaji pesa kiasi kutatua dharura zako. Unafika kwenye ATM unakuta hii maneno....unafanya nini, hasa ukiwa kilaza kama mimi.



Automated Teller Machine

Labels: