BARUA ENZI ZA MWALIMU
Naona kati ya huyu jamaa na huyu jamaa atakayetangulia kutuma barua hii atakubaliwa na Koero Mkundi
WAAMINIFU WANAAMINI BARAGUMU LIKIPIGWA LINA JAMBO, TENA JAMBO JEMA. BASI BARAGUMU HILI LINAJITAHIDI KUFIKIRISHA, KUFUNZA NA KUBURUDISHA
BARUA ENZI ZA MWALIMU
11 Comments:
:-)
Mie nakumbuka barua yangu ya kwanza ilinyunyuziwa na manukato halafu nikashindwa kumpa KIMWANA aliyekuwa ananitesa roho kisa moyo ulikuwa unadunda sana.
Halafu kwa bahati mbaya ikashikwa na dada yangu aliyetaka kunisaidia kufua nguo za shule halafu akaitembeza kwa ndugu zangu wote nyumbani kwa hiyo siri yangu ikawa imebumbuluka nyumbani.:-(
pole sana mkuu. lakini vipi sisteri hakukusaidia kupeleka ujembe kwa mhusika?
@ John: Zaidi ya kutaniwa sana sikupata msaada. Halafu tukahama Songea kwa hiyo ndio ikawa imetoka. Ila baadaye nilikuja kukutana na huyo kimwana ukubwani zaidi nikajikuta sikumbuki kwanini nilikuwa namuona bomba sana zamani. Kwa hiyo sikuhitaji tena kifuko chake cha dhambarau.
Halafu sijui kwanini WASICHANA wengi hubadilika haraka sana. Nishawahi kumpa shikamoo demu niliyesoma naye Primari kwa kuzania ni mtu wa makamo sana kunizidi.:-(
simeone ushawahi kufikiria kuandika kitabu ya hekaya ama hadidhi fupi fupi? au ushaandika? you have the stories that are required, man!!
Najaribu kuandika hekaya kadhaa! Ntakutumia uzicheki nikisha zipitia vizuri kwa mara nyingine.
kaka zangu nimecheka sana.
ukiacha zile za awali, barua maarufu ya kumwaga sera ili nipate tulizo la moyo kama siyo nafsi ilikuwa ni darasa la saba.
tulikuwa tushafanya mtihani wa taifa sasa tupo ktk maandalizi ya graduation.
nikajipinda nikaandika tenzi arobaini na mbili nikielezea hisia zangu kwa binti mmoja wa kichagga. alipoipata barua ile ambayo nyuma ya karatasi nilisihi asimwambie mtu, akamwita rafiki yake na kumsimulia.
stori zikaenea darasa zima hivyo kila mara nikawa nachekwa eti natongozea mashairi. hapakutosha na wala sikuwa na ujasiri wa kumwuliza yule binti kulikoni kamwaga mchele kwenye kuku.
nikaenda sekondari na kusahau habari zile za kukosa umaridadi pamoja na kujipinda koooote kule... nilitumia siku mbili kuidraft ile barua nikiamini kwa saundi zile dogo habanduki. aisee.
the fun thing...juzi hapa siku ya Idd si ndo nikakutana tit for tat na mwandikiwa mashairi yale baada ya miaka 15. kila mtu aliishia kucheka. swali lake la kwanza, "bado unaandika mashairi?"
unajua nilimjibu nini? nikamwambia, "unataka nikuandikie tena?"
ha ha ha ha ha aaaaaa nimekumbuka mbali sana maana naandika hii comment nikiwa hoi bin taaban kwa kicheko.
fadhy yako ni hadithi hai. kama nakuona unavyoandika hapa
Mhhh, kweli yakale yanaraha kuyasimulia, hasa enzi za shule! Nafikiri kama kungekuwa na namna ya kuhifadhi haya matukio kwenye kanda za video, tungenufaika sana `kinafsi'
Simon na Fadhy umeniacha ho kwa simulizi zenu ama kweli watu tunatoka mbali. Ila kwa kweli hata mie imenikumbusha mbali sana. Na sikumbuki ni lini nimepata barua ila tuache mchezo ni raha sana kipata barua kama hizo zilizoandikwa kwa mkono. Naona muda si mrefu hakuna mtu atayeweza kuandika kwa kutumia kalamu na karatasi.. Ahsante kwa kumbukumbu hii!!
Sisi kijijini kulikuwa na jamaa kabisa 'spesheli" kwa uandishi wa barua za aina hii. Tulikuwa tunamnunulia miwa, vitumbua na vitu vingine.
Umenikumbusha mbali. Mimi pia bado ninazo barua za aina hii katika makabrasha yangu; na mara moja moja huwa nazisoma. Maisha!
Mimi nilikuwa nikiandikiwa badala ya kuandika!
Post a Comment
<< Home