Monday, September 27, 2010

MTEMBEA BURE SI SAWA NA MKAA BURE

Leo nikiwa nafikiria nini nipost katika blogu hii nikagundua sina kitu kuanzia kichwani hata mtandaoni cha kuwashirikisha wasomaji wangu. Wakati najijifikirisha nilikuwa nasikiliza hiki kibao cha MUCHANA cha mchawi mwingine wa Kongo Kanda Bongomani. Nikaona niwashirikishe kuusikiliza kwa mara nyingine wimbo huu. Ila siwajui MAJINA YAO hao wadada wanaoitikia, wanaodakia na kucheza. Kuna anayewajua/wafahamu? Napenda sana muziki wa Kongo wa kuanzia 1996 kushuka chini. Huu wa siku hizi wa kia Fali Ipupa mbalimbali na mimi.
Kama unusikiliza sana muziki huu wa enzi za kabla ya 1996 utagundua kuna segment ya gitaa la solo kuachiwa litawale. Huwa nakipenda kifaa hiki hasa kikikunwa na anayekipatia kama Lokassa ya Mbongo hapo videoni.

Labels:

5 Comments:

At 6:46 AM, Blogger Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Nilikuwa jeshini Makutupora Kanda Bongoman alipokuja Bongo kwa mara ya kwanza. Watu walitoroka kwenda Bongo kushuhudia kwani jamaa alikuwa anavuma sana.

Gitaa la Solo walikuweko akina Dally Kimoko na Diblo Dibala. Gitaa linapigwa mpaka mwenyewe unalisikilizia kabisa. We acha tu.

 
At 11:17 PM, Blogger mwalyoyo said...

Umenikumbusha mbali sana ndugu Mwaipopo, enzi hizo muziki wa Congo ulikuwa muziki kweli. Siku ukija Dar tuwasiliane ili nikupatie hizo albamu nzima nzima za hao Wakongomani.

 
At 12:35 AM, Blogger SIMON KITURURU said...

Kibao kimetulia!

Mie kwa asilimia kubwa nimedakwa na oldies karibu katika kila genre ya musiki.Sijui ndio kuzeeka?:-(

 
At 5:39 AM, Blogger John Mwaipopo said...

solo la wakina dally kimoko, diblo dibala, lokassa ya mbongo, nene tchakou na akina franco linafanya mtu usahau majukumu kidogo

alex nikija dar the first thing kukupigia. ntazikomba album hizo nzimanzima

 
At 5:39 AM, Blogger John Mwaipopo said...

solo la wakina dally kimoko, diblo dibala, lokassa ya mbongo, nene tchakou na akina franco linafanya mtu usahau majukumu kidogo

alex nikija dar the first thing kukupigia. ntazikomba album hizo nzimanzima

 

Post a Comment

<< Home