Friday, October 29, 2010

TAKUKURU VILAZA?



Hii ni sehemu ya tangazo moja la TAKUKURU wakati huu wa uchaguzi. Mimi najiuliza hivi kuna sehemu zingine INARUHUSIWA kutoa rushwa?

Labels:

Tuesday, October 19, 2010

KUMEKUCHA UCHAGUZI

Katika kuhakikisha siiachi/siikosi haki yangu ya kupiga kura nikafungua mtandao wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi kujirishidha kuwa nimo ama simo. Wako systematic sana unaingiza namba ya kadi yako na mtandio unaonyesha hali ya uwepo (ama kutokuwepo) kwako. Pia unatumiwa e-mail. Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar ndio wako systematic zaidi. Zanzibar unajithibitisha kwa kutumia simu ya mkononi tu.



Kwa karibu zaidi



Kwa mbali kidogo

Labels:

Monday, October 18, 2010

MIAKA MITATU BILA LUCKY DUBE



Tarehe ya leo miaka mitatu iliyopita majahili walikatiza maisha ya lucky dube. Kisa? Gari. Naam gari la Lucky Dube lilikuwa bora kuliko maisha yake.

Huwa sichoki kumsikiliza Dube 'mwenyebahati'.

tumkumbuke tukisikiliza kibao chake "Let Jah be Praised"

Labels: