MTEMBEA BURE SI SAWA NA MKAA BURE
Leo nikiwa nafikiria nini nipost katika blogu hii nikagundua sina kitu kuanzia kichwani hata mtandaoni cha kuwashirikisha wasomaji wangu. Wakati najijifikirisha nilikuwa nasikiliza hiki kibao cha MUCHANA cha mchawi mwingine wa Kongo Kanda Bongomani. Nikaona niwashirikishe kuusikiliza kwa mara nyingine wimbo huu. Ila siwajui MAJINA YAO hao wadada wanaoitikia, wanaodakia na kucheza. Kuna anayewajua/wafahamu? Napenda sana muziki wa Kongo wa kuanzia 1996 kushuka chini. Huu wa siku hizi wa kia Fali Ipupa mbalimbali na mimi.
Kama unusikiliza sana muziki huu wa enzi za kabla ya 1996 utagundua kuna segment ya gitaa la solo kuachiwa litawale. Huwa nakipenda kifaa hiki hasa kikikunwa na anayekipatia kama Lokassa ya Mbongo hapo videoni.
Labels: kanda Bongomani