MADEREVA TEKSIWapendwa waaminifu wa kupitiasha macho bloguni kwangu karibuni. Nilipotea hewani kidogo kwa sababu mbili; mosi ni kutokuwa na mtandao na pili kusafiri. Nilikuwa dar kwa siku 5 hivi. Nikiwa mbali na mtandao nilibahatika kusoma shairi hili hapa chini kuhusu mateksi dereva. tufuatane na mshairi mwenyewe...
Madereva wa Taxi
Na John Nkurumah Makacha (Mteule) “man of vision”
Utafiti nilofanya, Tanga na Mwanza mjini,
Na mwingine kule Kenya, hasa Mombasa Likoni,
Hakika umenifanya, nigundue ni wahuni,
Madereva wa taksi , ni wahuni wa kutupwa.
Kulamba wake za watu, kwao sio mtihani,
Kwa kutoa lifti tu, huwapata kilaini,
Wenye wake kila mtu, tahadhari chukuweni!
Madereva wa taksi , ni wahuni wa kutupwa.
Madenti wa sekondari, huwekwa vimada ndani,
Zawadi ni usafiri, ili wawahi shuleni,
Na kutaka ufahari, wawajue wao nani,
Madereva wa taksi , ni wahuni wa kutupwa.
Wana vimada lukuki, ukiwapanga foleni,
Mara leo Mama Jaki, na kesho Mama Semeni,
Kwa ngono hawatosheki, hivi wamerogwa nini,
Madereva wa taksi, ni wahuni wa kutupwa.
Kila kona wamezaa, hawana nyota kijani,
Wakikatiza mitaa, nyimbo ni baba fulani,
Una haki kushangaa, ni watu aina gani?
Madereva wa taksi , ni wahuni wa kutupwa.
Ndipo mwalimu mkuu, Makacha mwenye visheni,
Biblia nanukuu, madereva kasomeni,
Malipo ya dhambi kuu, ni kuzikwa kaburini,
Madereva wa taksi , ni wahuni wa kutupwa.
chanzo: mtanzania machi 15, 2010
Labels: ukware