Kufanana, kufaana ama kufaa
Kufanana ni hali ya kitu ama mtu mmoja kuwa na sifa zinazoshabihiana na za kitu kingine ama mtu mwingine. Wakati fulani hata watu huweza kushindwa kuwatofautisha watu wafananao. Kwangu dhana ya kufanana ni ya kimaumbile tu na si ya maana zaidi ya hapo. Baadhi ya binadamu wamekuwa wakifurahia wao wenyewe ama mtu fulani kufanana na mtu mwingine aghalabu mtu mashuhuri ama tajiri. Mifano angalia hapa na hapa Mimi sichukii mtu kunanana na mtu lakini sidhani watu kufanana ni jambo la kupigiwa upatu pasi na kufikiri namna gani kufanana huko kuwe kwa manaufaa ya wote wafananao ama ya jamii kwa ujumla. Watu utawasikia huyu anafanana na rais wa nchi fulani, au mfanyabiashara fulani au mtu maarufu huyu ama yule. Mie huwa nadhani ni kupoteza muda. Mbona punda wa lioko kijijini kwenu wanafanana na wale walioko katika kijiji chetu na hawatambi wala kuwatambia watu kuwa wanafanana? Kwangu la msingi ni watu kufaana wao kwa wao ama kuifaa jamii nzima.
Labels: Musings


