Friday, November 06, 2009

Kufanana, kufaana ama kufaa
Kufanana ni hali ya kitu ama mtu mmoja kuwa na sifa zinazoshabihiana na za kitu kingine ama mtu mwingine. Wakati fulani hata watu huweza kushindwa kuwatofautisha watu wafananao. Kwangu dhana ya kufanana ni ya kimaumbile tu na si ya maana zaidi ya hapo. Baadhi ya binadamu wamekuwa wakifurahia wao wenyewe ama mtu fulani kufanana na mtu mwingine aghalabu mtu mashuhuri ama tajiri. Mifano angalia hapa na hapa Mimi sichukii mtu kunanana na mtu lakini sidhani watu kufanana ni jambo la kupigiwa upatu pasi na kufikiri namna gani kufanana huko kuwe kwa manaufaa ya wote wafananao ama ya jamii kwa ujumla. Watu utawasikia huyu anafanana na rais wa nchi fulani, au mfanyabiashara fulani au mtu maarufu huyu ama yule. Mie huwa nadhani ni kupoteza muda. Mbona punda wa lioko kijijini kwenu wanafanana na wale walioko katika kijiji chetu na hawatambi wala kuwatambia watu kuwa wanafanana? Kwangu la msingi ni watu kufaana wao kwa wao ama kuifaa jamii nzima.

Labels:

5 Comments:

At 1:42 AM, Blogger Bennet said...

Waungwana walisema duniani wawili wawili, ndio kufanana huko na mara nyingi huwa tunapenda kujifanannisha na vitu vizuri

 
At 1:18 AM, Blogger viva afrika said...

kujifananisha na mtu huo ni udhaifu lakini kama mtu anafanana na mtu mwingine sioni tatizo.

 
At 4:31 AM, Blogger Yasinta Ngonyani said...

Kufanana,kufananisha au kufaa nashukuru hayupo aliyefanana nami...LOL

 
At 4:45 PM, Blogger SIMON KITURURU said...

Nshawahi kufananishwa na Mwizi basi wacha nijitetee!:-)

Sasa ngojea ufananishwe na mume wa mtu kuwa niwewe uliokuwa unampunguza mkewe utamu wakati karudi ghafla wakati wewe hilo hujui uone!:-(

 
At 1:28 AM, Blogger poker said...

PROMO DELIMA
poker online | Agen Domino | Agen Poker|Kumpulan Poker | bandar poker | Judi Poker | bandar qiu | Judi online terpercaya

Bonus yang kami sediakan :
* TO (Turn over) sebesar 0.3% yang akan di kami bagikan setiap hari senin
* Bonus referal sebesar 10%

Ayo segera daftarkan diri anda dan bergabunglah bersama kami !!
Delimapoker.com Situs Agen Poker Online Terpercaya di Indonesia akan melayani Anda dengan profesional, memproses depo/wd dgn cepat.
Come join and be a winer with us !!

Untuk info selanjutnya silakan chat ke :
Livechat_____: delimapoker
BBM__________: 7B960959
Facebook_____: Facebook
Phone number_: +85595678845

 

Post a Comment

<< Home