Tuesday, April 14, 2009

Alipata Kusema ...

If you talk to a man in a language he understands, that goes to his head. If you talk to him in his language, that goes to his heart. Nelson Mandela.

(Ukiongea na mtu kwa lugha anayoielewa, yatamkaa kichwani. Ukiongea na mtu katika lugha yake, yatamkaa moyoni.)

Nimekutana na nukuu hii ya mzee wetu. Pengine moja ya vyanzo ya mifarakano na mitafaruku ni lugha gongana. Watu hatuelewani kwa sababu hatutimiziani, ama makusudi ama kwa sababu maalumu fulani. Hebu wape watu mkate uone kama wataingia mtaani kugoma. Hebu wape mikopo ya kueleweka uone kama wataenda DECI. (Benki sasa zimefikia hata riba ya 28%). Hebu wape watu vitabu na mazingira mazuri ya kusoma uone kama watakwiba mitihani. Hebu wape watu mishahara mizuri uone kaba watakuwa mafisadi (lakini fisadi ni fisadi tu).

Labels:

4 Comments:

At 1:49 AM, Blogger boniphace said...

kaka hii ni makala ndefu ambayo umeibana. DECI ni picha halisi ya umaskini na kwamba maskini amefikia hatua ya kutafuta mbinu zakew pekee za kumnasua. Mfano pale River Side kuna wauza magazeti. Wauza magazeti hawa hucheza upatu wao wa kila siku. Hawana sheria ya kuwalinda lakini maisha yao yamekuwa hivi hivi kila siku.
Deci inafumbua macho ya swali la ya wapi mabilioni yaliyopewa jina la JK? yALIENDA KWA AKINA NANI?

jE FEDHA za EPA zilitakiwa kwenda wapi? Nini hasa hofu ya serikali katika DECI? Je ni katika kuwaonea huruma wananchin ama ni hofu ya kutanuka mtandao ambao unaweza kuwaondoa madarakani kwa kuwa wameshindwa kupambana na umaskini kwa vitendo. Kwa mwoga huenda kicheko lakini kwa jasiri kilio? Upo wakati jamii duni itakataa kusikiliza kelele za usifanye hivi kwa kuwa wanaozitoa wana nafasi ya kufanyajambo lakini wameshindwa kufanya

 
At 2:09 AM, Blogger John Mwaipopo said...

Boniface hii ni reflection ya makala yako ya juma lililopita mle Rai. Maswali kuhusu DECI ni mengi kuliko majibu. Pengine hata vigogo walikuwamo. Pengine vigogo wanaogopa kuwa sawa kiuchumi na masikini. Wanaogopa kuwa hawatakuwa na wa kuwaongoza.

 
At 2:12 AM, Blogger Christian Bwaya said...

Kaka umenena. Nimekupata.

 
At 3:20 PM, Blogger Yasinta Ngonyani said...

Hapa nimejifunza kitu...!

 

Post a Comment

<< Home