Nani Zaidii?
Yvonne Chakachaka Mbilia Bel
Wakati fulani huwa najiona nina mambo ya kizamani hivi. Moja ya mambo hayo ni kupenda muziki wa zamani. Miongoni mwa wanamuziki wa zamani ninaowahusudu sana ni hao wakina mama, enzi hizo wasichana. Mpenda muziki yeyote anajua 'shuguli' ya hawa. Nikiwaweka katika kipimio changu Mbilia anapata asilimia 51 na Yvone 49. Mbilia Bel pamoja ya kuwa anatumia lugha ambayo kwangu ni kichina bado mirindimo yake inakosha. Huyo ni mimi. Wewe je?
Wakati unawaweka katika kipimio watazame katika nyimbo Faux Pas (Nia mbaya) Mbilia Bel
Let Him Go wa Chakachaka
P. S. Jumapili (13/12/09) nitakuwa safarini lakini ni siku njema kwangu kutimiza miaka kadhaa. Tufurahi sote.
Labels: kumbukizi