Tuesday, April 14, 2009

Alipata Kusema ...

If you talk to a man in a language he understands, that goes to his head. If you talk to him in his language, that goes to his heart. Nelson Mandela.

(Ukiongea na mtu kwa lugha anayoielewa, yatamkaa kichwani. Ukiongea na mtu katika lugha yake, yatamkaa moyoni.)

Nimekutana na nukuu hii ya mzee wetu. Pengine moja ya vyanzo ya mifarakano na mitafaruku ni lugha gongana. Watu hatuelewani kwa sababu hatutimiziani, ama makusudi ama kwa sababu maalumu fulani. Hebu wape watu mkate uone kama wataingia mtaani kugoma. Hebu wape mikopo ya kueleweka uone kama wataenda DECI. (Benki sasa zimefikia hata riba ya 28%). Hebu wape watu vitabu na mazingira mazuri ya kusoma uone kama watakwiba mitihani. Hebu wape watu mishahara mizuri uone kaba watakuwa mafisadi (lakini fisadi ni fisadi tu).

Labels: