Monday, June 23, 2008

Shilingi 100 ya Mmasai

Hii ya shilingi 100 nimeitoa Bagamoyo juma lilipopita.

Enzi hizo ningepata magazeti ya Ngurumo kumi. Shukurani ya picha kwa mdau Maggid Mjengwa


Labels:


TFF Mafisadi?

Rais wa TFF Leodgar C. Tenga

Jamani naomba mnisaidie hivi inachukua siku ngapi kuhesabu na kutangaza kiasi kinachopatikana kutokana na mauzo ya tiketi za kuingilia kiwanjani. TFF hawajatangaza mpaka leo kiasi cha mapesa waliyoyapata kutokana na mechi ya Tanzania na Cameroun Uwanja Mkuu wa Taifa. Ninajiwa na hisia za kaufisadi hivi.

Katibu wa TFF Frederick Mwakalebela

Hata hivyo viwango vya mechi hiyo vilikuwa juuu sana. Si haba walipata pesa ya kutosha ambayo pengine inawatoa udenda.

Labels:

Monday, June 16, 2008

Ikulu ya Kwanza Nchini
Jengo hili lililopo Bagamoyo ambalo ni kama gofu vile au mahame inasemekana ndiyo iliyokuwa Ikulu ya kwanza ya Tanganyika wakati wa Wajerumani kabla ya kuhamishia Magogoni.

Labels:

Kiswahili katika maandishi ya Kiarabu

Niliwahi kusoma sehemu ambayao siikumbuki kuwa Kiswahili kilikuwa na maandishi yake lakini wajanja wa kikoloni walikiweka Kiswahili katika herufi za Kirumi na watawalo wa kwanza wa nchi zetu hizi hawakutaka kurejea katika herufi za awali. Hata hivyo hazikuwa za Kiarabu kama hizi. Waarabu nao walitaka kuchomekea maandishi ya Kiarabu kama katika picha hii niliyoifuma Bagamoyo kwenye makumbusho ya Kanisa Katoliki.


Je kuna yeyote anaweza kututafsiria baadhi ya sentensi hapo?

Labels: