Saturday, May 29, 2010

HAKUNA TENA FEGI

Annivesary Zingine... sikiliza..


Fegi ni hatari kwa mvutaji

Keshokutwa 31/05/2010 ni siku ya kupiga vita matumizi ya bidhaa za tumbaku(Sio lazima kuisoma hapa na hapa). Bidhaa mashuhuri ya tumbaku ni sigara. Nilikuwa mvutaji mzuri sana wa fegi kwa miaka kadhaa hivi. Mwaka jana tarehe kama ya leo (29/05/2009)niliona share yangu ya kuvuta fegi inatosha. Naam sijatumia kitu hicho kwa mwaka sasa na sikusubiri siku ya kujaribu kuacha ama kupunguza. Kwa mnaoendelea kuvuta hebu fikirini upya kwa kupima faida na hasara. Hapa kwenye hasara nadhani hatubishani. Binadamu bila sigara inawezekana!

Dhima ya siku ya kuacha kuvuta sigara mwaka huu inalenga katika kupunguza matumizi hayo kwa wanawake. HAPPY NO TOBACCO DAY!

Labels: