Kwikwi ya Mtandao
kwa siku zaidi ya 12 nimekuwa sipati mtandao kutokana na sababu za kiofisi zaidi hapa ninapofanya kazi ya ushika chaki, mbeya lakini. Nimeshindwa kupata, kujibu na kutuma salamu za Krisimasi na mwaka mpya. Nanyakua fursa hii ya kupata mtandao leo kushukuru kwa maamkizi ya sikukuu hizo na mie kutuma za kwangu. Leo sitoki ofosini mpaka wanifukuze saa tano usiku hivi. Nasoma post za blogu zenu zoote nilizozikosa katika kipindi hiki cha 'giza'. Pichani nimeanza na salamu za siku ya kuzaliwa mtu.
P.S. hako kashati nilikotinga ndio kale nilikopiga nilipoanzisha blogu hii January2006 New Jersey Marekani. Angalia picha yangu ya utablulisho wa blogu. Nakazimia sana.
Labels: mtandao

