Tuesday, January 05, 2010

Kwikwi ya Mtandaokwa siku zaidi ya 12 nimekuwa sipati mtandao kutokana na sababu za kiofisi zaidi hapa ninapofanya kazi ya ushika chaki, mbeya lakini. Nimeshindwa kupata, kujibu na kutuma salamu za Krisimasi na mwaka mpya. Nanyakua fursa hii ya kupata mtandao leo kushukuru kwa maamkizi ya sikukuu hizo na mie kutuma za kwangu. Leo sitoki ofosini mpaka wanifukuze saa tano usiku hivi. Nasoma post za blogu zenu zoote nilizozikosa katika kipindi hiki cha 'giza'. Pichani nimeanza na salamu za siku ya kuzaliwa mtu.

P.S. hako kashati nilikotinga ndio kale nilikopiga nilipoanzisha blogu hii January2006 New Jersey Marekani. Angalia picha yangu ya utablulisho wa blogu. Nakazimia sana.

Labels:

8 Comments:

At 7:28 AM, Blogger Yasinta Ngonyani said...

Na kweli ulipotea mpaka tulikuwa na mpanga kukutangaza umepotea. Karibu sana.

 
At 7:54 AM, Blogger SIMON KITURURU said...

Karibu tena Mkuu!

 
At 8:12 AM, Blogger Bwaya said...

Mzee sijui nani wa kumkaribisha mwenzie maana nami nimekuwa nimo simo.

Nimelizimia shati lako mzee. Miaka minne liko bado jipya? Rangi hiyo naifagiliaga sana na nyeupe yaani we acha tu.

Nakutakia heri ya mwaka mpya. Mlongo mpya ndo hivyo tena umeanza!

 
At 1:43 PM, Blogger Mija Shija Sayi said...

Shati bado linakutosha?

 
At 1:53 PM, Blogger chib said...

Tulibakiza kidogo tuuu... Tutoe blog yako na picha kwenye vyombo vya habari ili utafutwe kwa zawadi nono.

Karibu tena mhesh

 
At 3:54 PM, Blogger Masangu Matondo Nzuzullima said...

Pengine katika kupotea ndimo mna kupatikana. Watu waliokuweko huko ulikokuwa umepotelea pengine walikuwa hawajui kwamba huku ulikuwa umepotea. Laiti kama tungekuwa na uwezo wa kuwepo katika sehemu nyingi kwa wakati mmoja!

Unakaribishwa na natumaini kwamba mwaka mpya (2010) umeuanza vyema!

 
At 1:38 AM, Blogger EDNA said...

Kashati kako bado kanang`aa kaka,na pole kwa matatizo ya mtandao

 
At 9:44 PM, Blogger mumyhery said...

Shati bado liko bomba

 

Post a Comment

<< Home