Thursday, December 30, 2010

SHUKURANI 2010


Mapozi Kijiweni

Napenda kujichukulia nafasi hii ya masaa haya machache kabla ya kuisha kwa mwaka 2010 kuwashukuru watu woote ndani ya blogu na nje ya blogu kwa yale mema yote waliyonitendea. Nashukuru kwa wao kufikiri nilistahili kutendewa mambo mema.


Kazi na Muziki

Nawatakieni wote wakati mzuri tukiusubiri mwaka 2011 kwa amani na upendo. Pia nawatakieni mwaka wa mafanikio na mabadiko chanya katika maisha yenu. Basi tukiusubiri mwaka ujao si vibaya tukajiliwaza kwa kumsikiliza na kumtazama SAM WA UKWELI katika songi lake hili SINA RAHA ambalo kwa mtazamo wa wengi limekimbiza sana miezi hii ya mwisho wa mwaka huu.



Kuna mistari fulani ya songi hili huwa siipati vyema utadhani kamimba kiyunani vile

alamsiki binuur

Labels:

Tuesday, December 28, 2010

SIJUI KUOKA MIKATE

Monday, December 20, 2010

MSHINDI BSS APATIKANA, LAKINI...



Mshindi wa shindano la Bongo Star Search 2010 ni Mariam Mohamed(pichani). Shindano lilifanyinka Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar-es-salaam mwishoni mwa wiki.

Kama kawaida Bongo Star Search haijakosa neno mwaka huu. Maneno ambayo yametawala vinywa vya wapenzi wa BSS ni uchakachuaji wa matokeo na lugha mbaya ya baadhi ya majaji.

Kuna hisia za uchakachuaji, tena mkubwa. Kutokana na jinsi ilivyokuwa inaonekana mshiriki mzungu alionekana kuvuta hisia za wapenzi wengi kuliko washindani wengine. Kama walivyokuwa wakisema majaji, mzungu Joseph Payne hakuwa mzuri sana katika kucheza lakini aliteka hisia kutokana na ubunifu wake na matumizi yake ya kiswahili. Washabaki ninaowafahamu walituma meseji nyingi sana kwa ajili ya mzungu. Takwimu za Jumapili ya kabla ya fainali zilithibitisha hili, tena sio kwa karibu. Joseph Payne alikuwa kawaacha wenzaka mbali sana. Tunaweza kusema kwa kuwa si mtanzania basi namna ilifanyika asipate mshiko wa 30,000,000/- lakini kumshusha mpaka nafasi ya tatu haikuwa haki. Kwa tulioangalia kupitia TV tulisikia waliohudhuria ukumbini wakimshangilia sana Joseph Payne alipoimba na walizomea (they booed) alipotangazwa mshindi wa tatu.

Kwa upande wa lugha za majaji kulikuwa na kukengeuka. Jaji mkuu alitamka wazi wakati shindano linaendelea kuwa Miriam Mohamed ndiye mshindi wake. Hili peke yake linaonyesha tayari mshindi alikwisha kujulikana. Iweje mshindi wa chief jaji ajulikane tayari huku wapiga kura tukiwa tunahamashishwa kuendelea kupiga kura.

Jaji Salama mwaka huu ameonyesha ukomavu. Kabla ya siku ya fainali michango yake imekuwa positive na inajenga. Alichemsha siku ya fainali aliposema kuwa endapo Joseph Payne angeibuka mshindi basi yeye (Salama) angejiua. Hii ina hisia gani?

Master J ni mzigo BSS. Ameota mapembe sasa. Siku ya fainali alisahau kuwa mashindano ya BSS yanahusisha watu kwa wao kupiga kura. Kumbe it involves other people’s money. Kama watu ndio walitakiwa kutumia pesa zao nilidhani maamuzi yao vivyo hivyo yangeheshimiwa. Wakati anamchambua Joseph Payne alisema watanzania ni washamba kwa kumpapatika mzungu. Huu kama si ubaguzi wa rangi ni nini? Sijui.

Nionavyo mimi hisia za uchakachuaji zipo.Mimi nadhani kwa kuwa mshindi anasemekana kupatikana kwa kutumia pesa za watu (sms), basi na iwe hivyo. Kama sivyo basi, BSS ifanye kama Miss Tanzania ambako tusio katika kamati hatuhusishwi na ushindi wa mtu na hivyo kutupunguzia namna yeyote ya kulala mika. Wakae tu kama kamati ya miss Tanzania na watangaze mshindi.

picha iko hapa

Labels:

Monday, December 06, 2010

YA KALE...
Leo nimeifukunyua hii picha. Nilipoiona nimecheka sana. Nimekumbuka mbali pia.



hapo ilikuwa novemba 2001 (kama sikosei) mimi na huyo mdada (siku hizi mmama)tulienda kujiunga na Kiongozi wa FM Academia kipindi hicho Ndanda Kosovo Kichaa. Ilikuwa Nkrumah Hall pale Chuo Kikuu. Nilikuwa kimbaumbau ukilinganisha na sasa.

Labels: