Tuesday, October 28, 2008

Yanga Bingwa 2009/2010
Mji woote huwa shwari tukiwafungaga hawa jamaa. Ni raha tulioikosa siku nyingi Lakini mla ni mla leo... Wangeshinda wao ungesikia vurugu na mitusi-mitusi mji. mzima.

Washabiki wakiwasubiri timu yao ije kuchinja mtuYanga kama timu ya taifa vile
Utani unapokolea balaa
Nguruwe keshachinjwa hapa na mpira ushakwisha


Wachezaji mamilionea wakitoka kuwashukuru washabiki baada ya Ben Mwalala kufanya mambo yaliyomleta nchini.



Full Shangwe "Wanaona haya mamefanywa vibaya"





Kibrazil-Brazil tu


Full shangwe plus.

Labels:

Friday, October 17, 2008

Mwaka Mmoja bila Lucky Dube
Kesho tarehe 18/10/08 tasnia ya muziki wa reggae itaadhimisha mwaka mmoja toka siku ile chungu ya kuuwawa kwa risasi wa nguli wa muziki huo wa kule africa kusini, hayati Lucky Philip Dube.
Akifanyaga vitu vyake watu walikuwaga nyomi. Sehemu nyingi ama ilikuwa wauane kwa kukanyagana ama ndugu wapoteane

Katoy kalikomponza hata majahili wakamtoa roho wakitaka utajiri wa fasta-fasta. Hapo ndio eneo la tukio alipojaribu kushindana nao na kisha kuugongo huo mti akiwa amekufa tayari.

Maziko yake. Tandiko majani, blaketi udongo.

Pengine alitabiri kifo chake katika wimbo Crazy World kutokana na uhalifu wa namna hiyo kukithiri Afrika ya Kusini. Ubeti mmoja unaenda hivi:

So far so good we still living today

But we don't know what tomorrow brings

In this crazy world

People dying like flies every day

You read about it in the news

But you don't believe it

You'll only know about it

When the man in the long black coat

Knocks on your door

'Cause you're his next victim

As you are living in this... (crazy world)

Kwaheri Lucky Dube

Labels:

Tuesday, October 14, 2008

Mabibo Hostel Kumekucha


Katika wiki hizi za kuwasili wanafunzi tayari kwa kuanza mwaka mpya wa masomo mambo huchangamka kupindukia katika hosteli hizo. Pichani mnazi ukiwa umetumika kutangaza aina anuai za biashara. Mabibo kunaboa sana wakati wa likizo ndefu.

Labels:

Taifa Stars 'walipolinda heshima'

Ukaguzi wa timu

Cape- Verde wakipasha

Watunza heshima wakipasha, Ivo Mapunda katika njano bahari (mpauko)


Mie nafikiri vinginevyo. Stars walipopoteza heshima kwani mpira wanaweza. tumbafu kabisa.

Labels:

Huyu ndiye Chifu Wetu Mwangupili

Wazee wa kule nilikozaliwa wamemtunuku Jk kuwa chifu wetu, Chifu Mwangupili. Tunuku hiyo amepewa jumamosi tarehe 11. Habari kamili hii hapa.

Labels: