Mwaka Mmoja bila Lucky Dube
Kesho tarehe 18/10/08 tasnia ya muziki wa reggae itaadhimisha mwaka mmoja toka siku ile chungu ya kuuwawa kwa risasi wa nguli wa muziki huo wa kule africa kusini, hayati Lucky Philip Dube.
Akifanyaga vitu vyake watu walikuwaga nyomi. Sehemu nyingi ama ilikuwa wauane kwa kukanyagana ama ndugu wapoteane
Katoy kalikomponza hata majahili wakamtoa roho wakitaka utajiri wa fasta-fasta. Hapo ndio eneo la tukio alipojaribu kushindana nao na kisha kuugongo huo mti akiwa amekufa tayari.
Maziko yake. Tandiko majani, blaketi udongo.
Pengine alitabiri kifo chake katika wimbo Crazy World kutokana na uhalifu wa namna hiyo kukithiri Afrika ya Kusini. Ubeti mmoja unaenda hivi:
So far so good we still living today
But we don't know what tomorrow brings
In this crazy world
People dying like flies every day
You read about it in the news
But you don't believe it
You'll only know about it
When the man in the long black coat
Knocks on your door
'Cause you're his next victim
As you are living in this... (crazy world)
Kwaheri Lucky Dube
Labels: kumbukizi
2 Comments:
Nimefuhia zaidi mimi natamani kuikomboa Tz
Lucky Dube alikuwa ni zaidi ya mwanamuziki, zaidi ya mwanafalsafa.
Ukiutafakari ujumbe ndani ya muziki wake, hakika nafsi yako itakiri kuwa dunia, si tu imempoteza mpiganaji mahiri, bali mwanafalsafa aliyebobea. Mwanafalsafa ambaye hakuchoka kuonesha njia.
Post a Comment
<< Home