Tuesday, May 27, 2008

Aaah Kumbe ???

Sishangai sana tabia za watu wa Afrika ya Kusini kuamua mambo kwa pupa pasi na kujaribu kuangalia pengine kuna namna mbadala ya kutatua matatizo. Sishangai na sitashangaa kuambiwa kuwa walishindwa kukaa meza moja na makaburu enzi zile za ‘uliokuwa’ ukiitwa ubaguzi wa rangi. Ndio maana walibugizwa marisasi. Sasa shida ya waafrika ya kusini sio rangi ni akili zao finyu. Hata viongozi wao hawaoni hili kama ni shinda. Rais na makamu wake wamechelewa mno kutambua hili tatizo na walipotambua hawakuonyesha kuwa ni tatizo kubwa. Eti ni dogo tu! Kufa watu 40 sio tatizo? Pengine ufinyu wa kutambua namna za kutatua matatizo ndizo zilizowafanya watawala wa kizungu kipindi kile cha nyuma kuwashona risasi wananchi wa Afrika Kusini. Kumbe tulifanya kosa kuwaonea huruma. Wao hawana huruma hata kidogo. Rais wa zamani wa Zambia Keneth Kaunda alisema shida sio ‘anti-white’ bali ‘anti-wrong’. Sio weusi wote nduguzo. Hatuna ndugu Afrika kusini.

Labels: