Tuesday, May 27, 2008

Aaah Kumbe ???

Sishangai sana tabia za watu wa Afrika ya Kusini kuamua mambo kwa pupa pasi na kujaribu kuangalia pengine kuna namna mbadala ya kutatua matatizo. Sishangai na sitashangaa kuambiwa kuwa walishindwa kukaa meza moja na makaburu enzi zile za ‘uliokuwa’ ukiitwa ubaguzi wa rangi. Ndio maana walibugizwa marisasi. Sasa shida ya waafrika ya kusini sio rangi ni akili zao finyu. Hata viongozi wao hawaoni hili kama ni shinda. Rais na makamu wake wamechelewa mno kutambua hili tatizo na walipotambua hawakuonyesha kuwa ni tatizo kubwa. Eti ni dogo tu! Kufa watu 40 sio tatizo? Pengine ufinyu wa kutambua namna za kutatua matatizo ndizo zilizowafanya watawala wa kizungu kipindi kile cha nyuma kuwashona risasi wananchi wa Afrika Kusini. Kumbe tulifanya kosa kuwaonea huruma. Wao hawana huruma hata kidogo. Rais wa zamani wa Zambia Keneth Kaunda alisema shida sio ‘anti-white’ bali ‘anti-wrong’. Sio weusi wote nduguzo. Hatuna ndugu Afrika kusini.

Labels:

2 Comments:

At 10:09 AM, Blogger Dotto Athumani said...

Hi there,
Nimelazimika kukujibu au kutoa maoni yangu katika thread yako ili tuwekana sawa, muda huu wakati natuma hii coment nipo Jiji la Johannesburg ambapo mauji na vitisho vya wageni wausi vimekuwa vikiripotiwa na vyombo vya habari. Kimsingi nilikuwa na mawazo kama yako kabla ya kujua ukweli lakini nimegundua kuwa wakati mwingine vyombo vya habari vimekuwa vikitujengea dunia ya kusadikika. Kwa mfano kwa jinsi suala la kufukuzwa kwa wageni lilivyovalia njuga limeiweka afrika kusini kama sehemu ya ubaguzi. Nimeongea na vijana wa aina tofauti hapa joburg na kiukweli hata wao wameefedheheshwa na namna vijana wenzao wachache ambao hawana shule, vibaka na majambazi walivyopotoka na dunia, si kweli wote hapa joburg wanapendekezwa na tatizo lililopo ila ni kikundi cha watu wachache ambao hawana muelekeo wa maisha wameamua kufanya hayo. Kama ulishwawahi kutazama filamu moja iliyotengenezwa hapa South Africa (TOTSI)utaelewa hali hii inakotokea.

 
At 6:19 AM, Blogger John Mwaipopo said...

Mnyadi thaanx for your comment. Ni vema sasa tunaweza kujua haya kutoka kwa ndugu zetu ambao nchi mlizotoka zilikuwemo kwenye idadi ya wasiotakiwa SA. Tunapopata hali isiyo ya hofu kutoka kwenu tunapungunza munkari.

Linalotu tutatiza na kutuudhi ni ukumya wa serikali yenyewe ya SA kusema haya mnayotuambia sasa. It took so long if, you can remember, for the govt to at least comment. The fgovt was silent. Hii ilitafsiriwa kuwa Serikali iliunga mkono kichinichini hao majambazi na wahuni wasio na shule. Tena serikali awali hikuomba msamaha mpaka mtu asiye serikalini Jacob Zuma alivyofanya hivyo. Govt to blame ndio uliokuwa msimamo wangu.

Hata hivyo nafarijika kujua hamtishiwi tena.

 

Post a Comment

<< Home