Saturday, May 01, 2010

MEI MOSI MBEYA


Leo nimeshiriki katika maandamano ya sherehe ya akina sie wa mwisho wa mwezi. dhima kuu mwaka huu ni kugomea waajiri mpaka kieleweke. Namfuata huyo dada wa mbele.


Ndani ya uwanja wa Sokoine


Katika pitapita ya kutafuta picha nikakutana na blogger wa siku nyingi Rashid Mkwinda (katikati)wa Fasihi za Ufasaha akisaka habari hapa na pale. Hapa alikuwa katika harakati za kumhoji mmojawapo wa wafanyakazi bora mwaka huu.


Jamaa wa Usangu Logistics (T) akikwea zawadi ya pikipiki kwa ajili ya ufanyakazi bora. Kushoto (nyekundu)ndio akina Usangu Logistics wenyewe.


Jamaa hawakukosa kutuonyesha namna wanavyotutengenezea kilaji. Mbeya kuna kiwanda cha TBL.


Huwaga sijivungi nikipata ya 'kuonja'.

Labels:

10 Comments:

At 8:24 AM, Blogger Yasinta Ngonyani said...

Mei mosi njema nawe kaka John. na wiki end njema. kumbuka sio ugimbi/ulasi mwingi..lol

 
At 9:19 AM, Blogger Fadhy Mtanga said...

Kaka Yohana naona ulikuwa unatamani masaa yaende fwasta mkajipongeze na wenzako pale Carnival..na siku hizi maji ya dhahabu yanatengenezwa Iyunga ndo basi tena.

Hongereni sana ndugu zangu wa Mbeya. Nimewaonea wivu maana mmependeza sana.

Ila ubovu wa uwanja wa Sokoine unakera sana. Na sasa hata katimu ketu ka Magereza kamefulia ndo basi tena.

Mecco, Silver, Tiger, Mbozi United, Tukuyu Stars, Prisons nk nk nk, sasa vimebaki historia 'na sisi tulikuwamo' vinatia uchungu kaka. Ngoja tu ninyamaze maana ntamwaga machozi.

 
At 2:20 AM, Blogger Akyoo said...

kaka nashukuru kwa kuweka picha by akyoo http://shaushi.blogspot.com

 
At 2:38 AM, Blogger John Mwaipopo said...

@ yasinta ngonyani asante ila nilipata hiyo moja tu si unajua walikuwa wanaonyesha ili kutamanisha!

bro fadhy mtanga mwamko wa soka mbeya umekuwa ukipungua siku hadi siku. sijui tumeingiliwa na pepo gani linalotufanya tusizipe tafu timu za mbeya. tumesahau mwaka 1987 tukuyu stars walikuwa mabingwa wa ligi daraja la kwanza tanzania (hakukua na ligi kuu kipindi hicho). watu wa mbeya tunataka kuona mafanikio ya kisika, hatujihusihi na kuwa chachu ya mafanikio hayo

magereza walishindwa kuwahamasisha wananchi wajione kama timu yao. yaani ilikuwa ya magereza kipesa na kiitikadi. wapenzi wa soka hatukuiona kama 'yetu'. prisons walishindwa kujipandikiza kwa washabiki kisaikolojia.

tukuyu stars ndio haimo hata kwenye hesabu siku hizi. nasikia iko daraja la tatu sijui la nne, hata huko nasikia ina adhabu ya miaka mitatu ya kutoshiriki mashindano.

labda prisons wata-bounce back. nimeongea na jamaa yangu ambaye ni insider wa prisons. wana mikakati ya kuirejesha mwakani. yetu macho na masikio

@ akyoo asante kwa kunitembelea na wewe ziweke zile zako tupate kumbukumbu nzuri.

 
At 11:07 PM, Blogger Born 2 Suffer said...

Nakumbuka wakati mdogo nipo shule tulikua tunaimba nyimbo ya sikukuu ya Mei mosi, Mei mosi mei mosi leo siku kubwa Tanzania.

 
At 2:04 PM, Blogger Mija Shija Sayi said...

Maandamano yamenikumbusha mbali sana CCM KIRUMBA Mwanza, ilikuwa raha si kidogo. Ila Mwaipopo umenifurahisha na hako ka'bia. Hongereni.

 
At 3:35 PM, Blogger Christian Bwaya said...

Mnaonekana vere vere siriaz na kuwabana waajiri. Sasa utuambie, mligoma?

 
At 4:18 AM, Blogger John Mwaipopo said...

tuliambiwa akili za kuambiwa na mgayua changanaya na zako kuepuka uwezekano wa kumwagiwa risasi za moto

 
At 5:01 PM, Blogger Christian Bwaya said...

Ha ha haaaa! Kuna mawili, ama Mgaya ndo kawatosa, au nyie ndo mmemtosa. Enewei. Ndo ilivyo. Mkwara kidogo kila mtu nyumbani kwake. Kazi ipo.

 
At 4:49 AM, Blogger Alex Mwalyoyo said...

hahahahhh!
Safi sana bwana 'PF', naona unakumbukia enzi za Isimikinyi, Ulefi, Kinyangesi na Itengule!
Tuko pamoja!

 

Post a Comment

<< Home