Wednesday, November 11, 2009

Ushawahi kukisikia Ki-Pidgin cha Nigeria?

Nimesomeshwa kuwa Nigeria kuna Kingereza-Kipidgin. Huzungumzwa na watu wa kati na wa chini (haimanishi wa juu hawakijui). Kingereza si kingereza ukijuacho wewe. Balaa tupu. Soma mifano hii:-
  • Wetin dey happen - means What is happening?
  • I no no, I no know, Me no no or Me no know - means I don't know
  • Come chop - means Come & eat
  • How Far? - means whats up? or hi
  • babe - means fine girl or chick
  • show - means meet up with me
  • Yarn or Yarning - means to talk
Kama unapenda kuelewa na kujifunza ki-pidgin hicho soma hapa kwa raha zako

Kama unapenda kusikiliza namna kinavyozungumzwa wasikilize P-SQUARE katika TEMPTATION (kong'oli video). Wameamua kutoka kwa kipidgin (klakini hii ni remix. ina rap (ghani) za kizungu nyingi). Kitu naufagilia wimbo huu ni kusheheni kipidgin. Wametoka kama mnigeria mewngine Amos Tutuola alivyoandika-ga The Palm-Wine Drinkard kwa kukutima kingereza 'chake mwenyewe'.


2 Comments:

At 8:30 AM, Blogger chib said...

Yeah Hawa jamaa wana lugha zao, mwaka jana jasho lilinitoka nilipojichanganya mitaani Lagos.
Jamaa alisema How-a day akiwa na maana ya how was your day!
N asi unajua lafudhi yao, utafikiri anaimba wimbo tena slow

 
At 2:14 AM, Blogger SIMON KITURURU said...

Wakati nafanya Masters niliishi nao sana hawa jamaa NA ndio mara ya kwanza kujua tofauti zao.

Nao watakuambia ni akina nani matapeli, malaya, au tu kwa kwenda shule kama ni Kenya Wajaluo.

Kwa bahati mbaya watu husahau katika kila mtu mweusi duniani ukutananaye kutokana tu na idadi ya watu weusi duniani , inawezekana mmoja ni Mnaijeria wakati wanafikiri Wanaijeria wote ni Matapeli.

 

Post a Comment

<< Home