Tuesday, November 03, 2009

Kasichana miaka 11 kajifungua Salama

Hivi pengine global warming inazidi kuongezeka kila mahali. Hivi sasa visichana vya miaka kumi vyaweza zaa pasi na matatizo ( angalia hata hapa). Kasichana haka ka Bulgaria Kordeza Zhelyazkova (pichani)kamejifungua salama mtoto wa kilo 2.5 na baada ya muda kakatoroka kwenda kumalizia sherehe yake ya harusi. Baba mtoto ana miaka 19. Malizia stori nzima hapa

Labels:

7 Comments:

At 8:52 AM, Blogger chib said...

Heeee, kazi ipo sasa!!!

 
At 4:38 PM, Blogger Candy1 said...

mmh...yangu macho tu maana mmh...haya

 
At 7:06 PM, Blogger SIMON KITURURU said...

Hii kasheshe sasa!
Ila tukumbuke wakati mababu zetu hawatumii miaka kama kipima umri, Kipimo cha afaaye kuzaliswa ilikuwa kuvunja ungo na ukubwa wa titi. Kwa hiyo wale wafanikishao swala hilo haraka usishangae kuwa labda wengine walikuwa kimiaka wadogo kuliko huyu.

Au pia labda ndio maswala ya kula kuku wa kizungu siku hizi a.k.a vyakula vya kisasa ambavyo fulu makemikali vifanyavyo toto dogo kuwa na kubwa eneo.

 
At 8:40 PM, Blogger Mzee wa Changamoto said...

Well!! Ni kama pilika za KUVUNJA REKODI ziko kotekote.
Nasubiri under 10 ajitokeze na mwana hapa
Tunaelekea kuzaa watoto wenye mimba. Yaani miezi tisa Baba anakuwa na mjukuu
Hahahahaaaaaaaaaa.

 
At 6:55 AM, Blogger chib said...

Simon na Mzee wa Changamoto.... ha ha haaaaa

 
At 1:20 AM, Blogger viva afrika said...

ulimwengu hauishi kunishangaza kila uchao!

 
At 3:10 AM, Blogger kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

sawa

 

Post a Comment

<< Home