Tuesday, November 17, 2009

Sio vibaya tukikumbuka

Kombe la Dunia ndio hiloo linanukia takriban miezi 7 bado.....


Huyu ni Sunday Oliseh (1974). Kiungo mshambuliaji wa Nigeria. Pamoja na mambo mengine, anakumbukwa zaidi kwa goli lake la volley katika Kombe la Dunia la mwaka 1998 dhidi ya Hispania. Awali Hispania waliongoza baadaye Nigeria wakasawazisha na kuwa 2-2. Goli hili la Oliseh (angalia videoni chini) lilikuwa mkuki wa sumu na ambalo Hispania hawatalisahau kwani liliwanyima kusonga mbele katika hatua ya pili na badala yake Nigeria kufika huko.

Labels:

7 Comments:

At 8:44 AM, Blogger chib said...

Mwaka ujao, watu wengi wana wasiwasi sana na mwenyeji kama atafanya vizuri.

 
At 8:46 AM, Blogger chib said...

This comment has been removed by the author.

 
At 4:55 AM, Blogger John Mwaipopo said...

hata mimi nilikuwa na wasiwasi na afrika ya kusini ila gemu walilopiga mwezi wa sita katika kombe la shirikisho linatia matumaini kidogo.

mie hudhani ili nchi za afrika (hii ya sisi weusi, sio ile ya waarabu) zifanikiwe kisoka lazima kuwe na vurugu hivi au hata vita. angalia ivory coast na congo kulikuwa ama kuna vita lakini wanafanya vema. afrika ya kusini ilitoka katika vurumai ya ubaguzi wa rangi ikawa bingwa wa africa (1996), miaka miwili baadaye ikawa ya pili (1998), miaka miwili baadaye (2000)ikawa ya tatu na kutokomea katika chati. ubora wa soka lao umekuwa ukiporomoka jinsi demokrasia inavyozidi kushamiri.

 
At 5:25 AM, Blogger chib said...

Ha ha haaa John!! Basi Maximo aende huko Tarime kwa akina Wanchari na Wanchoka akachague timu ya Taifa.

 
At 9:38 AM, Blogger Mzee wa Changamoto said...

Durudishe ubaguzi ili soka inyanyuke nini?? Labda demokrasia inaendana na KUFICHANA MAOVU. Inaendana na KUDHULUMU PESA ZA KUENDELEZA SOKA, labda INABEBA MAFISADI WANAOSHINDWA KUTUMIA KILA WANACHOPEWA KUISAIDIA TIMU na kama ilivyo kwetu, labda SIASA INAINGIA KWENYE MICHEZO kwa kuwa tu tuna WAZALENDO.
Tutafika ila sijui ni lini????

 
At 11:43 PM, Blogger Upepo Mwanana said...

Nashukuru sana kwa kunitembelea. Karibu tena, nami nitakuwa mgeni wako mara kwa mara

 
At 3:34 AM, Blogger viva afrika said...

japo kuna wachache wanaodai yapo mabadiliko ya dhati katika soka la tanzania, bado nina mashaka na mikakati ya kuhakikisha tunaenda hizo world cup zijazo, mbuyu ulianza kama mchicha.

 

Post a Comment

<< Home