Kufanya Mitihani na Mimba
Serikali imesharuhusu wanafunzi 'waliteleza' kufanya mitihani ya mwisho. Juzi wameanza wa darasa la saba. Nafikiri mwendo ndio huohuo kwa kidato cha nne na cha sita.
Hivi ni faida zipi na hasara zipi tuzitarajie kwa ruksa hii?
Picha kutoka kwa michuzi
Labels: education
6 Comments:
Naamini faida mojawapo ni kuwasaidia waliobebeshwa kijaza dunia kuweza kujiendeleza kirahisi kielimu baada ya kumaliza kusaidia kuujaza ulimwengu
Tunatakiwa kuachana na adhabu bali wale waliokosea wanahitaji kurekebishwa, hii ndio njia moja wapo lakini inabidi tuwe makini kidogo
Haraka haraka haina baraka . Tutafika tu huko. Ila mi sijaelewa kwa nini wasichana wanaobeba mimba wasiendelee na masomo yao kama kawaida au baada ya kuzaa?
Kama wa kiume wanaachwa kufanya mtihani, kwa nini hawa wa kike wasifanye? Tabia zao zinafanana, isipokuwa huyu wa kike anabeba kidhibiti!
Bwaya! Weye una akili sana
Faida ni kuwa hata ambao walikosea wanaweza kupata nafasi ya pili kujirejea. Na kwa kuwa wanakuwa na "chungu" ya maisha, wanaweza kuwa makini zaidi.
Hasara ni kuwa wasio na akili wataona kuwa hawana la kuhofia (japo si ukweli) kwa kuwa tu hata wakipata mimba watasoma.
Kuwatisha na kuwaadhibu kabla ya kuwaelimisha ni kutwanga maji
TUWAELIMISHE WAJITAMBUE NA KUTAMBUA HASARA NA ATHARI ZA MATENDO YAO
Blessings
Post a Comment
<< Home