Wednesday, June 17, 2009

Mjengo wetu Baaab Kubwa
mbali na kuwa kiuchumi tuko nyuma kwa mbali saaaaaana ya Uingereza, na pengine nyuma kidogo ya Kenya lakini jengo letu la Bunge ni balaa. Kubwa kichizi. kweli usafi au umaridadi huonyesha si masikini, au?


Hili La Uingereza


Hili la Kenya


Hebu Cheki letu. Lipi Kali?

Labels:

6 Comments:

At 3:07 AM, Blogger Born 2 Suffer said...

Yaah la Bongo limekaa poa sana kwa nafasi na usafi kila mbinge anachukua raha yake, La Uingereza finyo sana kwa nini?

 
At 12:00 AM, Blogger Egidio Ndabagoye said...

Kaka bongo mjengoni humo hamna wanalofanya zaidi ya kusinzia na kukuza vitambi.

@Born 2 suffer wenzetu hawaingii bungeni kujiachia,wako pale kwa akzi maalum na kwa muda fulani sisi wale walaghai wanakwenda kusinzia mule.

 
At 8:30 AM, Blogger Bwaya said...

Ukiangalia kwa haraka haraka huwezi amini kwamba lile ndogo lenye watu waliobananaaaa ndilo lililojadili namna ya kuwasaidia wale waliokaa kitajiri waliochepusha matumizi ya misaada ya waliobanana.

Hapo ndipo umasikini wetu unapokuwa bayana: Unatumia hela za mtu anayeishi kikawaida halafu unaishi kitajiri kuliko hata huyo aliyekusaidia.

Fukara bwana ana mengi. Bora ufukara wa hela kuliko ule wa juu ya mabega.

 
At 9:15 AM, Blogger John Mwaipopo said...

Egidio karibu tena maana tulidhani ushapotezwa haiderabad (sijui nimepatia?)Ila siku hizi hawasinzii Star TV na TBC zitawaumbua. mbunge akijisikia kulala siku hizi wanaingia mitini kabisaaa. bola lawawa kuliko ....

Bwaya kama kawaida yako una mambo. karibu tena kwani nawe kama ulipata ka-vakesheni hivi?

 
At 6:57 AM, Blogger Bwaya said...

Naam kaka. Saa nyingine twabanwa mbavu, tunakuwa kama twakosa pumzi si unajua tena kaka?

Ila sasa sharubati yangu naipatia nikitazama mablogu yetu.

Nsharudi mkubwa.

Naomba kamsaada fulani cha lugha. Hebu durusu pale kwangu uone namna ya kunisaidia mjomba.

 
At 12:55 AM, Blogger mwalyoyo said...

Natarajia kuna siku na ww utaingia mahali hapo, nitakuwa msitari wa mbele kukusaidia ufike!

Kazi njema

 

Post a Comment

<< Home