Sunday, March 12, 2006

Twaweza Kujivuna Kifua Mbele Kuwa Sisi ni Nani? Mavazi Yatosha.

Alan wasaalan wapendwa wanablogu za Kiswahili. Leo nimekuwa bussy kidogo na vijishughuli vyangu hapa mtoni. Laini sio sana maana ufundishaji wangu hapa ni kama niko likizo fulani vile. Nina wanafunzi wachahe ukifananiaha na wale wastani wa 500 ninaokuwa nao kila mwaka pale kijiweni kwangu Mbeya (zamani DSA).

Nimekuwa na wakati mgumu hapa Marekani kwa masuala kadhaa. Mengi ya hayo ni kawaida inapokuwa unabadilisha tamaduni na mazingira. Bahati njema mengi nemeshayazoea na sasa na dunda kama 'kawa' tu. Kwa mfano masuala ya kutafuna misosi yao hii lilikuwa taabu tupu. Lakini sasa natafuna tu pasi na matatizo.

Langu leo sio geni sana. Lahusiana sana na hii hali ya hewa hapa Marekani ya kaskazini. Kwa kawaida sehemu hii ya nchi ni baridi sana kuliko kule kusinikusini aliko Boniphace Makene, lakini sio kama baridi ya kule aliko mpare huyu. Makene aliniambia-ga huwa-ga anavaa-ga kaptura tu na kuingia mtaani. Thubutu kuvaa kamptura hapa New Jersey halafu uingie mtaani. Unaweza kushangaa ghafla umezingirwa na gari la zimamoto, gari la wagonjwa na na lile la polisi kwani 'msamalia' mmoja anaweza kuwa amewapigia simu na kuwaambia kuna 'punguani' sehemu fulani. Kitakachofuatia sio maswali bali ni msobemsobe mpaka Intensive Care Unit kukupima ubongo na akili yako. Mpaka kugundua kuwa wewe si hamnazo ni tuu leti.

Pengine hili ni kati ya yale mauza-uza ambayo abadani sitaweza kuyazoea hapa Marekani ukizingatia kuwa hata hivyo wasaa wangu wa kusalia hapa umebaki mfupi tu. Si punde nitakuwa Dar ama Mzizima kucheza Twanga Pepeta (Original au Chipolopolo) nikiwa njiani kupitia Mikumi, milima mizuri ya Udzungwa na Kitonga kuelekea jijini Mbeya.

Baridi haizoeleki ati. Hata wazawa wa hapa si tu hawaipendi bali pia wanaichukia kama nini. Je itakuwaje kwa mpitanjia kama mimi.

Nilipokuwa nakaribia kuja huku Marekani sikuelewa vema mabalaa nitakayoyakuta hasa kuhusu hii baridi Nikabeba vijinguo vyangu ninavyovaa-ga Dar na Mbeya. Nikakusanya vishati vyangu vya batiki, tena vya mikono mifupi. Hata hivyo niliwahi kupata fursa yakuvivaa kabla dholuba haijatamalaki pale Novemba. Nilichelewa kuyavaa yale mashuka ya kimasai ingawaje mimi ni (bashiri mwenyewe).

Ninachotaka kujadili hapa ni utambulisho tunaokuwa nao miongoni mwa watu wa mataifa mbalimbali kutokana na mavazi yetu. Nakumbuka wazungu wakizimia vivazi hivi na kusema, "Your shirt is so beautiful John." Hawakuishia hapo: "When you go back to your country I need two like those." Nikawa nimefanikiwa kupeleka ujumbe.

Juma la pili akaja jamaa mweusi kama mimi nilipokuwa nimekaa. Alijawa na bashasha dhahiri kuniona. Kabla hata ya kunisalimia swali lake lilikuwa: "Where in Africa do you come from brother?" Baadaye ndipo akaniambia kuwa anatoka Nigeria. Mavazi yangu ndio pekee yaliyomfanya anitambue natoka wapi. Hakika kichwa kilivimba wakati ule kabla ya msimu wa baridi haujaanza. Nguo zote unazozipenda zinakuwa ndani ya koti zito, pengine usizivae kabisa kwani hazitangamani na makoti yao hapa. Mnigeria mwingine aliyevaa kama Rais Olusegun Obasanjo (pichani juu)aliniambia kule Washington kuwa mavazi ya kikwetu yanatutofautisha na kutuonyeasha sisi ni kina nani na wapi twatoka.

Siku moja tukibung'aa bung'aa jijini New York jamaa mmoja wa kutoka Israel akanishawishi nininue fulana imeandikwa "I love New York." Kuepusha shari nikamwambia "Siipendi New York ila kama utaniuzia iliyoandikwa 'I love Jerusalem' au 'I love Tel aviv' nitanunua."

Napenda sana mavazi ya kikwetu kama hilo alilivaa Da'Mija Shija (pichani kushoto, kwa hisani ya albamu yake). Pia hebu angalia ninavyotofautiana na huyu mlezi wangu hapa mtoni (pichani chini ya hiyo ya Olusegun). Vyetu vizuri jamani na tuvipende basi walau mara moja moja. Yafaa nini sisi tuwe kama hatuna kwetu wakati watu wa kutoka mfano China, Nigeria, Uarabuni na kwingineko wanawakilisha.

10 Comments:

At 12:56 PM, Blogger boniphace said...

Sera nguimu sana Baragumu. Lakini kama mkulima wa Pamba wa Musoma Vijijini anakosa soko la pamba yake lazima mimi mwananchi wa hapo nipige vita avazi ya nje nivae yangu ili kutanua soko. Siku hizi fikra zangu ni uchumi kwanza siasa baadaye. Haya mavazi bomba tu ni kutaka ukuu ndio maana kulipuka Kizungu zungu wakati hata wao hawalipuki hivyo katika kazi zao. Kuna kazi kwetu ya kupenda mavazi yetu na vitu vingine tunavyozalisha wenyewe. Tukivichukia nani avipende? Jeff hapa upooo maana naamia hii ni imani yako na Baragumu amegusa kabisa ikulu.

 
At 6:37 AM, Blogger mloyi said...

Baridi likizidi kuwa mjanja kuliko mbuni! unajua mbuni kwenye jua kali huwa anafukia kichwa chake chini ya ardhi. sasa wewe baridi likizidi tengeneza duara la moto ulale kaitkati yake moto ndio uwe ukuta wako!
Muisrael anakuuzia fulana ya "i love newyork"! na wewe umetoka kwenu na shati kama la damija! lililotengenezwa india na kitambaa chake kushonewa darisalama kwenye kile kiwanda cha MwarabuMhindi ambalo faida yake itatumika kumsomeshea mtoto wa kiasia anayesoma kule Canada- harakati umewahi kumuona?- ili akafanye kazi uingereza.
Utamaduni ( ulio duni?) unatumika kutambulisha na kuipa heshima jamii, utamaduni ni wa wote katika jamii sioni sababu ya utamaduni wa kiafrika kuwa ghali sana kwa mwafrika! Kama wewe unamudu kununua kitu cha kwetu na wengi hatuwezi hicho sio chetu tena, ni cha wale wenyekukimudu!.
nguo hizo ni mzuri ila hazipo kwa wote. Inabidi waliojua hili azitoe kwa wote.

 
At 12:09 PM, Blogger Jeff Msangi said...

Mwaipopo,
Hii mada ni tamu sana.Kama alivyosema Makene hii ni imani yangu kabisa.Nathamini sana vitu kutoka kwetu.Naamini kwamba uafrika ni kitu chenye thamani sana.Nikikiachia nitakuwa nimeachia lulu na kukamata majani.Mavazi kimekuwa na kinaendelea kuwa kitambulisho changu muhimu sana hapa Canada.Infact kimenijengea heshima kuliko nilivyotarajia.Kinachonisumbua ni kwamba hamna makoti na majaketi ya kuzuia baridi ya kiafrika.Hivyo wakati wa majira ya baridi huwa sina budi kutinga haya haya ya kwao ingawa ndani mwake huwa bado napeperusha utambulisho wa nitokako kwa mavazi.
Tusiishie kwenye mavazi tu,lazima tusukume mbele fikra zetu pia.Akikuambia neno mjibu neno.Ajue kwamba wewe si mnyonge wala mtu wa mzaha.Mzungu akiingia kwenye gari langu au nyumbani kwangu basi ajiandae kusikiliza midundo ya kwetu,ale chakula cha kwetu na ikibidi ajifunze kula kwa mkono ili pilau linoge zaidi.Najua siku nikirejea nyumbani baadhi ya watu watashangaa kwamba sina fubu,sean john nk.Majibu yao ninayo!
Mwaipopo,mwendo ni huo huo.

 
At 7:42 AM, Blogger MICHUZI BLOG said...

sina uhakika kama nitaungana na wasemaji waliotangulia pamoja na wewe john. nadhani si makene aneyependa kuvaa suti na tai kila siku, ama jeff ambaye koti lake la kutokea usiku halimtoki. bila shaka twafahamu utofauti wa hali ya hewa ughaibuni na huku kwetu, na pia matabaka ambapo ukiangalia tu suti ya mtu unamjua huyu ni wa tabakla lipi. sidhani kama john ulitoka nje na hiyo wax baada ya kumaliza warsha hiyo, na hata kama ulifanya hivyo aidha ilikuwa kiangazi ama koti lilikuwa lakusubiri sehemu yake pale mlangoni. hata mimi ukinikuta nimekula suti huku utagutuka kidogo, kwani hilo joto acha!

 
At 6:56 AM, Blogger Christian Bwaya said...

Jambo hili niliwahi kukumbana nalo katika kisebule cha Ndesanjo. Awali sikuwa naelewa umuhimu wa mavazi ya Kiafrika. Nikajikomboa.

Ni vizuri kama nini kujionea fahari na vitu vya kwenu. Mavazi yana sehemu kubwa katika utambulisho. Hapo umesema kweli. Hongera kwa mtazamo huo Mwaipopo.

 
At 3:41 PM, Blogger Ndesanjo Macha said...

Mwaipopo, shati zuri sana. Ni furaha kuona ukituwakilisha. Mzee Olesegun, pamoja na siasa zake mbovu, huwa ananifurahisha na mavazi yake. Jerry Rawlings naya alikuwa akiwakilisha nchi yake kimavazi. Gaddafi wa Libya naye siku hizi badala ya kuvaa kiarabu anavaa majoho ya Afrika Magharibi kupalilia siasa zake za "Afrika Moja."

Kulikuwa na makala moja kwenye gazeti la New African wakati fulani. Makala hiyo ilisema kuwa waafrika wanapokuwa wamevaa mavazi yao wakifika viwanja vya ndege ughaibuni huwa wanachukuliwa kama vile ni wana wa wafalme. Nakubaliana na makala hii. Kuna heshima kubwa sasa tunapata tunapovaa mavazi yetu maana bila kuficha ni mazuri sana na ni ya kipekee.

 
At 3:51 PM, Blogger Ndesanjo Macha said...

Wapo watu wanaomini kuwa ukivaa suti unapewa heshima kubwa. Inaweza kuwa dunia imelazimisha, kupitia vyombo vya habari, tamaduni-maarufu,n.k., kuamini kuwa suti ni vazi la hadhi ya juu kuliko yote duniani (ndio maana harusi bila suti inaonekana imechuja). Lakini tusisahau kuwa kuna watu ambao huwa wanafikiria nje ya mkumbo. Picha ya Obasanjo na Powell, kwa mfano, nikiambiwa nichague katika nguo walizovaa, nitachagua za Obasanjo. Sipendi sana tabia ya kumeza mambo na mitazamo bila kuitazama imeanzia wapi na kuishia wapi. Hii mitazamo inayofanya kila kitu cha hadhi ya juu kiwe kimetoka nje ya utamaduni wangu nitaikataa hadi nitakaposhawishiwa vinginevyo. Mitazamo kuwa majina yanayotamkika vizuri ni yao, nguo za hadhi ya juu ni zao, miziki mizuri ni yao, lugha zenye hadhi ya juu ni zao, imani za kidini na mitume ya kweli ni vyao vyote. Mitazamo hii ina historia yake, ukiimeza bila kujua nafasi yake katika historia ya ukandamizaji wa mtu mwenye ngozi ambayo sio nyeupe utakuwa umetumbukia kwenye shimo ambalo Marcus Garvey alilifahamu ndio akasema, "mtu asiye na ufahamu wa historia na utamaduni wake ni sawa na mti usio na mizizi."

Kabla sijamaliza, naomba niseme wazi kuwa sisemi kuwa mtu asivae suti au kanzu na kofia yake. Ukipenda mavazi hayo vaa. Ila muhmu sana ujue ni kitu gani kimefanya kukawa na "makubaliano fulani" kuwa mavazi hayo au lugha fulani ni bora kuliko mengine au lugha nyingine.

 
At 5:45 AM, Blogger Rama Msangi said...

Mwaipopo hapa umenigusa kwa ukaribu sana maana suala hili linanihusu mno, na kabla sijaendelea kusema machache nikuahidi kuwa nitazungumzia kuhusu suala hili kule ukumbini kwangu, utakaribishwa kusikiliza mazungumzo yangu.

Mwaka juzi, nilipokuwa kule Dodoma, kulianza suala fulani hivi ambalo liliendeshwa kimya kimya lakini kwa kasi kubwa na ya aina yake (sio mpya lakini), kama lilivyokuwa Azimio la Zenji.

kalikuja kamradi fulani kaliitwa ka kutafuta vazi la taifa, kakala tumilioni kadhaa twa Wabongo, kisha vazi la 'Chon-lai' ambalo naambiwa asili yake ni Uchina, likatangazwa vazi la kitaifa baada ya kuibuka kidedea katika kashindano hako.


Watu wakalaani sana na kuhoji kulikoni, lakini kama ilivyo ada, Sirikali ikakaa kimya na kusema huo ndio mwongozo wa kulipata vazi la kitaifa. Ukafuata muda wa watu kusubiri kuibuliwa rasmi kwa vazi la Mtanzania, toka wakati huo hadi leo hii hola, hamna kitu, suala lile limekufa kimya kimya kama Azimio la Arusha nadhani

Lakini ndugu yangu Mwai, nashukuru kuwa kamradi hako kaliibua vipaji vipya katika masuala ya mitindo ya mavazi na kipaji kimojawapo kilichoibuka siku hiyo kilikuwa kwa kijana mmoja aitwaye Ramadhani Msangi (Unashangaa!! Kalaga baho)

Tukutane barazani kwaku siku nitakapojadili suala hili na picha za kijana huyu siku hiyo

 
At 9:29 PM, Blogger Pusat Perkasa said...

vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada

 
At 1:35 AM, Blogger poker said...

PROMO DELIMA
poker online | Agen Domino | Agen Poker|Kumpulan Poker | bandar poker | Judi Poker | bandar qiu | Judi online terpercaya

Bonus yang kami sediakan :
* TO (Turn over) sebesar 0.3% yang akan di kami bagikan setiap hari senin
* Bonus referal sebesar 10%

Ayo segera daftarkan diri anda dan bergabunglah bersama kami !!
Delimapoker.com Situs Agen Poker Online Terpercaya di Indonesia akan melayani Anda dengan profesional, memproses depo/wd dgn cepat.
Come join and be a winer with us !!

Untuk info selanjutnya silakan chat ke :
Livechat_____: delimapoker
BBM__________: 7B960959
Facebook_____: Facebook
Phone number_: +85595678845

 

Post a Comment

<< Home