Monday, January 31, 2011

MALANGALI: KUSANYIKO LA TULIOSOMA HUKO


Wanafunzi wakiwa mbele ya Ukumbi wa chakula na Mihadhara

KUTAKUWA NA KUSANYIKO LA WATU WOTE TULIOSOMA SHULE YA SEKONDARI MALANGALI KWA AJILI YA KUFAHAMIANA NA KUJADILI MASUALA YA PAMOJA NA MAENDELEO. KUSANYIKO LITAKUWA TAREHE 5/2/2011 SAA 9 JIONI CHONYA INN (RIVER SIDE)MBELE KIDOGO YA LANDMARK HOTEL UBUNGO, UKITOKEA UBUNGO. TAFADHALI TUJULISHANE WENGINE. MAWASILIANO PIGA 0787525396

Labels:

9 Comments:

At 5:06 PM, Blogger kassim said...

duuh, mbona hujaweka hata picha yetu? MGL hoyeeeeeeeeeeeeeeee

 
At 5:07 PM, Blogger kassim said...

Kaka ningekuwa bongo ningetia timu, ila niko mbali mnooooooo. Hivi STONEY DIS yupo nchi hii?

 
At 4:30 AM, Blogger Yasinta Ngonyani said...

Hakika ni jambo la maana sana bahati mbaya mimi sikusoma huko. Kila la kheri....

 
At 8:32 PM, Blogger mwalyoyo said...

Tuko pamoja Kaka. Nitakuwepo

 
At 3:47 AM, Blogger John Mwaipopo said...

Kassim i hear uko UK, very good. hata mimi niko mbali niko mbeya lakini watakayoyajadili nitajitahidi kuyarusha hapa hapa tuone kama yana mbolea

kuhusu picha nilitafuta iliyo readily available online. za kwetu sikuscan

yasinta tuko nawe kifikra

mwalyoyo utatujulisha yatakayosemwa huko

 
At 3:55 AM, Blogger kassim said...

tuko pamoja kaka, usisite kutujulisha yatakayojili.

 
At 1:48 AM, Blogger SIMON KITURURU said...

Mkutano mwema!

 
At 11:17 AM, Blogger kassim said...

Kikao cha wana MGL kiliendaje? Tupeni feedback wadau

 
At 2:42 AM, Blogger mwalyoyo said...

..Ingawa nilikuwa na udhuru siku hiyo ya kikao, lakini nilipata dondoo kwa ufupi kama ifuatavyo:-

Hakika kikao kilikuwa kizuri sana, kulikuwa na umati wa 'Wanamalangali' kama 40 hivi. Kamati ya muda ya kuratibu mkutano huo iliteuliwa, ikiongozwa na Stan Nyavanga na wenzake. Walianza kwa kukumbushana mazingira ya sasa ya shule na kuangalia mahitaji ya sasa ya shule yetu.

Makubaliano:
1. Kuunda kamati rasmi ya kutathmini changamoto zinazoikabili shule kwa sasa na kuangalia namna ya kukabili changamoto hizo (ikiwemo kushuka kitaaluma katika maka ya hivi karibuni)
2. Kuunganisha wanafunzi wote waliosoma Malangali kwa njia ya mtandao na njia ya ana kwa ana (ili kuwapa fursa hata wale walio mbali na Malangali) kupata taarifa za mara kwa mara na kuchangia maendeleo ya shule.
3. Kuitisha mkutano mwingine mapema iwezekanavyo ili kuanzisha 'Alumni' ambayo itakuwa na katiba rasmi na uongozi rasmi kwa ajili ya kushughulikia changamoto za shule.
4. Kuwakutanisha wana Malangali angalau mara moja kwa mwaka
5. Kuanza kuchangia ununuzi wa vitabu vya kiada na ziada na kuvikabidhi shuleni kwa utaratibu utakaopangwa, ili kukuza taaluma. Lengo ni kuongeza vitabu ambavyo tumesaidia kuvichakaza kwa elimu tuliyonayo ili wadogo zetu nao waweze kusoma.

Maazimio hayo yatajadiliwa zaidi katika kikao kijacho.

Mwalyoyo

 

Post a Comment

<< Home