Wednesday, May 03, 2006

Miujiza ya Ki-Yesu Yesu Bongo

Nani kakwambia ni Yesu pekee aliweza kufanya miujiza ya kugeuza mikate na samaki wachache na kuwa chakula cha maelfu. Nani kakudanganya ni Yesu pekee alifufua wafu, kuponya wagonjwa na miujiza mingine lukuki. Bongo kuna muujiza umetokea wa kujenga shule zipatazo 381 kwa miezi minne tu! Sio kuendeleza zilizokuwapo. Hapana. Mpya 381 ndani ya miezi minne!. Kama unabisha fungua hapa.

15 Comments:

At 9:33 PM, Blogger Mija Shija Sayi said...

Mbona hawakutueleza zimejengwa wapi na wapi na majina yake ni yapi?
Nina swali hapa, tumeongeza shule na waalimu je?

Asante kwa kutuletea miujiza hii ndugu Mwaipopo.

 
At 1:18 AM, Blogger mzee wa mshitu said...

Hapa ndipo utakapokuja kushangaa nyingi zimejengwa sawa, lakini tujiandae watoto wetu kuangukiwa na baadhi ya majengo hayo si zaidi ya miaka mitano ijayo ni kwamba watu wamekula hela ya saruji wakaweka mchangayiko dhaifu, sijui walimu watawapata wapi ikiwa hivi sasa kuna upungufu wa zaidi ya asilimia 35 ya walimu wa shule zote. Hizo zitafunzwa na nani?

 
At 1:41 AM, Blogger mwandani said...

Idadi kubwa sana kwa miezi minne nadhani, nami niulize kama mija: ni shule za namna gani?

 
At 7:21 AM, Blogger Jeff Msangi said...

Habari hii nadhani inanipa utata fulani.Mwaipopo,unaweza kutuchunguzia zaidi?

 
At 10:00 AM, Blogger Ndesanjo Macha said...

Nimeamua kuwa Tomaso aliyetaka kugusa makovu ya misumari mkwenye viganja vya yesu. Eti shule ngapi kwa miezi mingapi?????
Isije ikawa haya yote ni mapambio ya vyombo vya uongo ambavyo vingi vimegeuka kuwa ni wasemaji wa rais.

 
At 12:28 AM, Blogger mloyi said...

Zimejengwa kweli tena kwa mtindo wa ari mpya nguvu mpya na kasi mpya. Ila wapinzani kama da'mija wanaendelea kutoziona. Tatizo sasa ni walimu na wanafunzi! Kumbuka kuna wazazi wanaofurahia watoto wao kutopata nafasi za sekondary sasa watakuwa wanapata. na kwa walimu kila mwalimu huwa anasema huu ni mwaka wangu wa mwisho kufundisha.
Kazi bado ipo,

 
At 12:58 AM, Blogger mwandani said...

Mloyi, Shule za namna gani hizo?
Miezi minne shule 300 na,

Shule hizo ni majengo ya pupa ya JKT au shule kama vituo vya kutoa elimu?

 
At 6:02 AM, Blogger Ndesanjo Macha said...

Mwandani, hata mimi bado nina swali kama lako. Mloyi, hebu tupeni habari kamili kamili. Shule hizo ni kwamba zimemalizwa kujengwa na serikali mpya (ila zikianza kujengwa huko nyuma?) au zimeanzwa na kumalizwa hivi majuzi? Mia tatu na?

Sio kwamba tunapinga, au tunasema haiwezekani. Habari kama hii ni vigumu kutoshangaza watu wengi.

 
At 6:26 AM, Blogger Ndesanjo Macha said...

Mwandani, hata mimi bado nina swali kama lako. Mloyi, hebu tupeni habari kamili kamili. Shule hizo ni kwamba zimemalizwa kujengwa na serikali mpya (ila zikianza kujengwa huko nyuma?) au zimeanzwa na kumalizwa hivi majuzi? Mia tatu na?

Sio kwamba tunapinga, au tunasema haiwezekani. Habari kama hii ni vigumu kutoshangaza watu wengi.

 
At 11:45 AM, Blogger boniphace said...

hii habari tusiimalizie hapa. Baragumu jaribu kuiendeleza kwa kusaka source zako tuipate ili tuiweke katika siku mija za JK maana ni tukio kubwa sana hili. Lakini kaka Charahani wewe ndiye uko chunguni huko hii habari tusomeshe tujue ukweli maana kudanganyana hatutaki kabisa

 
At 12:28 AM, Blogger Reggy's said...

Sina shaka na hizo shule kuwepo. Nina sababu na mifano: Shule hizo hazikujengwa mahali pamoja na wala hazikujengwa na serikali kuu kwa kodi za wananchi. Kama ujuavyo kila halmashauri ya wilaya, miji na Manispaa inajitegemea na inajenga shule zake. Je, kila halmashauri ikijenga shule mbili tu, kwa maana ya madarasa ya kuingiza wanafunzi wapya wa kidato cha kwanza, jengo la utawala, vyoo na samani, itashindikana vipi kupata shule 381?

Mfano hapa Dodoma, Janauari watoto 6,146 walichaguliwa kuingia sekondari kati ya 12,859 (47.8%) na baada ya miezi mitatu, Machi mwishoni zilipatikana nafasi 3, 520 baada ya kujengwa shule mpya na kuongeza madarasa katika baadhi ya shule za zamani, hadi hapo waliochaguliwa wamefikia 80.2 ya waliokuwa wamefaulu. Mfano huu ukizungushwa nchi nzima, aliloandika sauti ya Baragumu ni muujiza wa kweli. Hoja inabaki ya Charahani 'mzee wa mshitu' kuwa hizo shule zinaweza zisiwe imara au ile ya Mija Shija Sayi kuwa huenda walimu hawatakuwepo. lakini pia, kauli ya serikali juu ya walimu, ilisema kwa sasa imeondoa usahili ili kuwavuta waliosomea ualimu miaka ya nyuma kuingia moja kwa moja, imehamisha walimu wote wa diploma kutoka shule za msingi ili wafundishe sekondari na imeanzisha 'UPE' ya aina nyingine ambapo wanahitimu wa kidato cha sita wanapigwa msasa wa wiki kadhaa na kuingia mashule kupiga chaki.-RSM-

 
At 12:07 AM, Blogger Maisha said...

this country is amazing...haya sasa tusubiri tu isije kawa nguvu ya soda.mimi nfurahia jinsi rais wetu mpya anavyotu-suprise na utendaji na utekelezaji wake.aichoke tu.maana akipata sapoti ya kutosha kutoka kwa team yake tutaona mabadiliko makubwa sana au kama alivyosema Sauti mwenyewe "miujiza" ya ajabu kabisa.ila kwanza awashughulikie hawa majambazi...

 
At 7:33 AM, Blogger Sultan Tamba said...

Bongo kwa siasa za midomoni!! Hawatuwezi!! Hizi ni siasa! Tatizo tunajenga nchi kwa mdomo ndio maana tuko hapahapa! Hawa wana siasa hawa hiyo siku ya mwisho watatuchelewesha sana sisi wenye pepo yetu kwa midhambi yao!!! Maana kesi zao zitakuwa ndeeeeefu kuliko sisi wenye kesi ndogondogo!! Mimi hata sifikirii mara mbili, hizi ni siasa za Bongo, hamna ukweli hapa!

 
At 3:47 AM, Blogger Indya Nkya said...

Tutofautishe shule na majengo au na madarasa. Kilichojengwa ni shule au madarasa?

 
At 1:35 AM, Blogger poker said...

PROMO DELIMA
poker online | Agen Domino | Agen Poker|Kumpulan Poker | bandar poker | Judi Poker | bandar qiu | Judi online terpercaya

Bonus yang kami sediakan :
* TO (Turn over) sebesar 0.3% yang akan di kami bagikan setiap hari senin
* Bonus referal sebesar 10%

Ayo segera daftarkan diri anda dan bergabunglah bersama kami !!
Delimapoker.com Situs Agen Poker Online Terpercaya di Indonesia akan melayani Anda dengan profesional, memproses depo/wd dgn cepat.
Come join and be a winer with us !!

Untuk info selanjutnya silakan chat ke :
Livechat_____: delimapoker
BBM__________: 7B960959
Facebook_____: Facebook
Phone number_: +85595678845

 

Post a Comment

<< Home