Wednesday, May 17, 2006

Kwaheri Marikani

Hivi leo namalizia rasmi maisha yangu hapa kwa Dubya. Heri safari ndefu ya maisha haya imegota salama na kwa amani. Maulana ashukuriwe. Panapo majaaliwa nitakuwa nikiblogu kutokea hapa katika jiji hili. Ni upande mwingine wa shilingi tu.

Alamsik Binuur

14 Comments:

At 11:51 PM, Blogger Reggy's said...

Karibu Sana Bongo. nakukaribisha bongo, nyumbani ili tugawane yaliyopo, hata kama ni matatizo. natarajia utaendelea kublogu kila siku, kusoma na kuchangia katika blogu za wengine kama ulivyokuwa umezoea, ingawa natambua fika kuwa huenda hilo lisiwezekane, lakini bila shaka utajitahidi. KARIBU SANA!

 
At 12:11 AM, Blogger Mija Shija Sayi said...

Tunashukuru umeanza mbio na kuzimaliza na sasa naona unajiandaa kwenda kuanza zingine.

Tunakutakia maisha mema na utusalimie Msangi Mdogo ukifika.

 
At 12:21 AM, Blogger Mija Shija Sayi said...

Samahani nilisahau kutoa wosia,

Mwaipopo halahala "juisi ya ndimu" (Gongo) usiende ukaifakamia maana nilisoma kule kwa Msangi Mdogo kwamba ukifika tu cha kwanza Gongo.

 
At 3:44 AM, Blogger mloyi said...

Unakuja nyumbani, vizuri, lakini hapa maisha ni mabaya sana, ujue nauli sasa ni Shs 250.00, sijui uliacha ngapi? mishahara ileile ya Mkapa, kikwete anasema tungojee matokeo ya tume aliyounda! Sijui kama tutaweza kuonana mara kwa mara.
Ombi Kijiwe hiki bado tunakihitaji ili tuwe na uhakika wa kuwa wote siku zote.

 
At 3:41 PM, Blogger boniphace said...

Nilisubiri upande ndege na sasa uko hewani nimefurahi kufanya nawe mazungumzo ya mwisho mwisho ukiwa bado hapa kwa Kichaka, tangu umeingia katika harakati hizi za Magazeti Tando umekuwa chachu kubwa tu na imani yangu ufikapo Tanzania utaweza kuwaingiza wengi zaidi kumiliki magazeti, redio na luninga tando zao kama ambavyo Ndesanjo amekuwa akihamasisha utanukaji wa teknolojia hii.

Ni imani yangu ufikapo Mbetya tutasoma muongezo wa Azimio la Dodoma na safari hii Mkwinda, Nyembo na Msangi na wengineo wa huko mwaweza kuwa na kikao kikubwa tu, tena hapo Chuoni kwako katika somo unalofunza waweza kuwafunza wanafunzi wako umuhimu wa kuwasiliana kutumia magazeti Tando na ukawapa extra credit wale watakaofungua yao.

Kisha, nikutakie heri na mapinduzi mapya katika mchakato wa kuingia katika siasa za nchi yetu. Huu kijana bado na waweza kufanya mema ukitilia maanani mafunzo uliyojifunza kwa kichaka na namna njema ya kutopenda mali za muda mfupi na za njia ya panya! La muhimu niombe tena kuwa harakati za kutaka kuweka maandishi yako pale Citizen zisiishie huku nenda sasa ongea na jamaa hapo na mkute Charahani ukifika Dar es Salaam, ili muweze kukutana wanajumuiya wa Dar es Salaam na kisha kutupa maelezo ya namna tunavyoweza kujenga jamii yetu.

Sijamaliza bado jamani, niongeze na hili, najua una kamera nzuri tu, sasa zile picha za watu wa cini kwa nini nazo zisipate fursa ya kung'aa na kupandshwa chati katika Gazeti tando lako? Unadhani hatutazipenda/ Thubutu tunazimisi sana, usisahau kuwasalimu wananchi jimboni kwako kila upatapo fursa wasalimie na wakumbushe kujitegemea wao kwanza na kuogopa misaada na mikopo. Waweza wakumbusha pia kujitahidi kuzalisha chakula, ni kila afikapo kiongozi wa serikali usiishie kumsifia, mwambie kile ambacho watanzania wengi hapo nyumbani hawawezi tena kukenua vinywa vyao na kusema, waambie tumechoka maneno twataka matendo, thatutaki rushwa na hatuoni raha kuutazama viongozi wetu wakijinufaisha na kusahau raia maskini! Wakumbushie pia kuwa Tanzania ni kubwaaaa na haiishii Dasalama tu, wafike Kujunjumele nako kuna shida na kunaishi watanzania wanaohitaji ukombozi. Sijamaliza bado, mengine si tutaandikiana na kisha kuwekeana mawazo humu! Kwa nini nisitamke kuwa mwaka huu nilipata rafiki ambaye hata wanangu walio kiunoni wakizaliwa wataweza kumuita baba pia? Hili lapaswa kufichwa au kuanikwa tu? Cheza karata yako inawezekana!

 
At 2:39 AM, Blogger mwandani said...

Kila la kheri, usiwache kutupasha habari kwenye blogo ukifika nyumbani.

 
At 3:40 AM, Blogger Christian Bwaya said...

Karibu tena nyumbani mwalimu. Ila ujue kuna njaa kali.

 
At 2:52 AM, Blogger Sultan Tamba said...

Hakuna maisha yaliyo rahisi na mazuri dunia nzima kama nyumbani kwenu! Hasa kama hakuna vita. Tanzania hakuna vita, ni salama salimini. Karibu mahali ambapo una haki zako zote za kimsingi. Ugenini ni ugenini. tu

 
At 2:23 AM, Blogger lucas said...

karibu nyumbani kaka..
walisemaga wahenga "nyumbani ni nyumbani hata kama kichakani...."

tunahitaji nguvu na utaaramu hata ujuzi pia ulioupata huko ..ili tuendeleze taifa kwa " KASI MPYA NA GUVU MPYA + ARI MPYA..."

KARIBU7 NYUMBANI

 
At 8:50 AM, Blogger Vempin Media Tanzania said...

Karibu Bongo ndugu yangu ukipata nafasi pita katika kijiji chetu hapa tunapatikana wakati wote tunashukuru kwamba umerudi salama maana mambo ya osama siku hizi mabaya sana

 
At 12:59 PM, Blogger Jeff Msangi said...

Mwaipopo,
Nadhani nikiongeza maneno mengine nitakuwa natia chumvi.Kajenge nchi..na sisi tuko njiani.Wamarekani wanaheshimu sana watu kama wewe.Mnaingia na muda wenu ukiisha mnarejea makwenu na sio kuanza kuishi kama digidigi.Kwa mtaji huo unaweza rejea Marekani siku yoyote utakapotaka wewe mwenyewe.Kila la kheri.

 
At 9:20 AM, Blogger Ndesanjo Macha said...

Mwaipopo, najua kuwa huu sio mwisho wa kublog. Pengine hutablogu mara kwa mara lakini unajua kuwa sauti yako tunaihitaji. Nchi inaihitaji. Vizazi vijavyo vinaihitaji.
Tupo pamoja kaka!

 
At 11:51 PM, Blogger ned said...

Mwaipopo
sina uhakika kama nimechelewa... lakini kila la heri mzee!
Wengine pia tupo njia moja!!!
Nafahamu waliopo Bongo wanaweza wasielewe... lakini ukweli ni kuwa
East or west home is best!
Kulia kushoto Bongo bomba!

 
At 9:02 PM, Blogger Unknown said...

Thanks for meaningful article...

 

Post a Comment

<< Home