Saturday, May 06, 2006

Hii Imekaa Vipi
Majuzi ilikuwa siku ya uhuru (ama ufungwa) wa vyombo vya habari duniani. Martha Mtangoo na Reginald Miruko walikuja na machapisho bloguni kuhusi siku hii. Suala kuu litandalo mawazo ya wanahabari ni kuwa je kuna uhuru kweli ama vinginevyo. Kama uhuru huo umenyakwa nani basi anaunyaka serikali ama waandishi wenyewe. Je, tuzilaumu serikali kupora uhuru huo ikiwa fika tunafahamu kuwa, kwa mfano Tazania, vyombo hivyo kwa urali fulani vimegeuka visemeo vya serikali badala ya chachu ya kuuliza kwa niaba ya wananchi. Kupigia baragumu serikali hasa kwa yale hata yasiyostahiki sio hatua ya awali kujipora wenyewe uhuru huo. Lakini pia mnamkumbuka Hayati Katabalo?
Huo ulikuwa mwanzo tu wa kuingia katika katuni hizi hapa chini kuhusu suala zima la uhuru ama ufungwa wa vyombo vya habari. Nimezifuma katika kusakasaka masuala mbalimbali mtandaoni. Unajua tena unapokuwa huna la maana sana la kufanya.
Unamkumbuka Chakubanga? Zake na nyingine nyingi tu za watanzania wenzetu zinapatikana hapa.

Alamsik Binuur.

5 Comments:

At 12:00 AM, Blogger Maisha said...

interesting stuff...im too obsessed with myself to write in the way you do but your blog is really good...

 
At 2:38 AM, Blogger Ndesanjo Macha said...

kungekuwa na blogu enzi za Katabalo...wewe! Natamani sana watu waliokuwa wakimfahamu kwa karibu ndugu Katabalo waandike habari yake kwa undani. Habari nyingi juu yake huwa zimeandikwa kijuujuu. Huyu bwana ana nafasi yake katika historia ya habari za kikachero Tanzania.

Kuna wakati uhuru wa habari unapotea kutokana na maguvu ya serikali, lakini kuna wakati mwingine serikali inaweza isifanye chochote kwani vyombo vinakuwa na utamaduni wa kujipendekeza.

 
At 11:56 AM, Blogger MICHUZI BLOG said...

ndesanjo umegusa pahala. hayatikatabalo atakumbukwa kwa kuwa mwandishi wa kwanza kuweza kuandika yale awali yalionekana matakatifu (kufichua maovu). niko safarini kuelekea brazil,nikirejea nitafanya utafiti na kutoa habari za katabalo kwa kina

 
At 12:04 AM, Blogger jen said...

John, asante kwa kuangalia blog yangu. Nafurahi unaipenda. Mimi ninaipenda nchi yako. Bado siwezi kuongea kiswahili vizuri lakini ninajaribu tu. Kila siku ninajifunza zaidi! Wanafunzi wangu wananisaidia: ninawafundisha kuhusu afya, na wananifundisha Kiswahili. Wanafunzi wa shule za sekondari wanahitaji kuongea Kingereza TU kwenye vipindi vya kawaida…lakini ninawaomba tuongee Kiswahili kwenye kikundi chetu cha afya. Nafikiri inabidi waelewe kila kitu, na nimeona wanafunzi wa kidato cha kwanza (na wengine pia) bado hawawezi kabisa Kingereza. Basi tunaongea Kiswahili na wanafunzi wananisaidia kutafsiri kama siwezi kueleza kitu fulani. (Pia ninajaribu kujifunza Kimakonde. Ngumu sana! Je, wewe unatoka mkoa gani? Kabila gani?) Nimesikitika kidogo kwa sababu siwezi kuelewa blog yako vizuri. Bado! Nitaendelea kujaribu kwa sababu nafikiri unaandika kuhusu vitu maalum.

 
At 11:45 PM, Blogger Reggy's said...

Mwaipopo na wenzako hapo juu, mmechunguza na kutoa lililo kweli kabisa. Katuni zimenifurahisha na nimetembelea site ya kina Kipanya www.africaserver.nl/bongotoons na kubaini nyingine, ikiwemo inayomwonyesha mwandishi akitishika kwa kivuli kikubwa cha serikali, lakini serikali inajitetea kuwa 'Mimi sina shoka, nimesimama tu nyuma yako'.

Ninachojiuliza ni kwanini serikali inasimama nyuma ya mwandishi wa habari? Inataka kufanya nini?

Pili, Suala la Katabalo 'katabaro' (sijui ni lipi) ni jambo kubwa sana na linahitajika hata wakati huu, lakini tukumbuke kwamba baada ya mtu huyo, mungu ailaze roho yake mahali pema, watawala walijidhatiti zaidi kuhakikisha vile visheria vilivyoku vimelala vinaamka na kufanya kazi.

Mifano, Jaribu kukumbuka suala la Adam Mwaibabile na nyaraka zake zenye muhuri wa SIRI (1997) lilivyomuonjesha kifungo, Suala la Majira na Rada feki iliyokuwa imenunuliwa (1994), Shaba na barua za kumbana Mrema wakati wa uchaguzi(1995) na vitisho hivyo, vimeendelea hadi hii leo, check issue ya ThisDay na Kulikoni against Manji (sh 100bn lible case) au ThisDay na Kulikoni againist Mkumbwa Ali, Ag MD of The Daily News (sh 1bn libel case) and many many others.

tatu, Lakini tusiishie hapo, kuna la zaidi, 'greasing newsgate' ambapo baadhi ya waandishi wameamua kujikomba kwa serikali, baadhi wakidhani watakuwa miongoni mwa wateule wa Rais, wengine kwamba wataendelea ku-enjoy ziara za president na PM (hiyo ni njaa binafsi).

Lakini je, kila anayeandika habari ana elimu ya kumwezesha kutambua anachotakiwa kuandika? Si wote. Kumbuka tangu enzi na enzi shule za waandishi wa habari TZ zilikuwa 2 tu TSJ na Nyegezi (zote ngazi ya Diploma hadi siku za karibuni, ambapo digrii zimeanzishwa. Vyomvo vya habari viliporuhusiwa kwa mkupuo mwaka 1992, waandishi walipungua sana (hawakutosha) baada ya kugawanyika; viliibuka vyuo vya wiki 2, mwezi mmoja, hadi miezi mitatu ili kusaka waandishi wa kutosha soko. Na kwa kuwa waandishi waliojiunga katika mkupuo huo hawalipwi vizuri hadi leo, wengi wao hawaweze kujiendeleza kielimu na waajiri wao hawawaendelezi. Hivyo uhuru wa Habari utaendelea kuwa mashakani. SAMAHANI KWA KUANDIKA MAREFU.

-RSM-

 

Post a Comment

<< Home