Saturday, May 27, 2006

Blogu ya Mazingira Imefumika

Alan wa saalan wanablogu na wasomaji blogu. Ukimya uliojitokeza ulishadidiwa na safari ndefu kutoka Paterson, New Jersey hata Dar es Salaam, Bongo. Bado inaendelea kuelekea Mbeya.
Bongo shwari hakuna shari. Pengine majambazi yamehisi kuwa wenye pesa zao sasa ni waangalifu zaidi. Pia yawezekana majambazi hayo bado yanakula faida kwanza.
Kufika Bongo nikakutana na rafiki yangu Alexander Mwalyoyo kashawishika na kukata shauri kuanzisha blogu ya Mazingira. Yeye hataki kuitukanisha taaluma yake ya mazingira. Sasa mazingira ndio nini na yanafaa nini katika kublogu. Mie maamuma lakini nikamtembelea Mtanganyika huyo hapa ili kujua vema.
Wakatabahu.

12 Comments:

At 11:14 PM, Blogger Reggy's said...

Pole na safari. Nilifungua hapa mara 10 bila kukuta chochote. Nilielewa kuwa bila shaka ulikuwa ama safarini au kule Mbeya umekwenda kwanza kijijini. Karibu Bongo

At 6:16 AM, Blogger mloyi said...

Karibu kama umeshafika. Bongo kama ulivyoiacha? Mwambie Makene na Ndesanjo nini wanachokosa. Vipi una matatizo kidogo na lugha yetu?, aha, wewe tulikuwa wote sio kama wale jamaa wanaotangazwa na FBI kwamba wameiba vifaa vya kompyuta, hivi hawakukusumbua pale Mwl. Nyerere Int. Airport? hawakukuulizia wale jamaa kama uko nao? tuambie ukweli, Uliwahonga dola ngapi? Angalia usiyazoee hayo!
Uko Mbeya tunatarajia sasa kupata mambo ya Mbeya kwa undani.

At 1:36 AM, Blogger John Mwaipopo said...

Wazee wa kazi nashukuru kwa ukaribisho. Nipo jijini Mbeya kama nilivyoahidi. Bahati njema nimekuta wamenitunia kibarua changu. Sijui Mbeya inanipa nini. Sifikirii wala kuwaza kuhama Mbeya kwa hivi kaibuni.

Kaka Miruko sijaingia mtandaoni kwa siku kadhaa kwa sababu kuu mbili ambazo kinamna zimawea kuwa moja: Kukiwa na umeme hakuna mtandao (network), kukiwa na mtandao hakuna umeme, ingawaje Mbeya haina matatizo sana ya umeme.

Mloyi: Nilipofika JKN eapot sikupata kukaguliwa hata chembe. Wajihi wangu uliwafanya wale jamaa wasinikague badala yake wakaanza-ga kuniulizaga masuala ya kina Njaidi. Sijui kwa nini sikubeba 'unga'. Hakika sikusumbuliwa hata chembe.

At 1:38 AM, Blogger John Mwaipopo said...

At 11:18 PM, Blogger Ndesanjo Macha said...

Ndio John. Najua unaweza usiwe na muda wa kuandika mara kwa mara kwa sasa. Ila ukipata wasaa utuangushie mistari miwili mitatu. Tupe habari za Mbeya.

At 12:09 AM, Blogger mwandani said...

Mwaipopo mzima?

At 3:25 AM, Blogger John Mwaipopo said...

Mwandani:Walahi namshukuru mwenyeenzi mie ni mzima pengine wa afya tele isipokuwa mjumuiko wa kujisetiri ikamilifu hapa nyumbani mbeya unanifanya nisionekana mtandaoni mara kwa mara. Pili ni kanchi ketu haka. Unapopata wasaa wa kwenda intaneti ujue utakuta moja kati ya haya manne 1) kuna mawasiliano (good), 2) hakuna umeme ila pengine mawasiliano yapo(balaa), 3)hakuna mawasiliano ila umeme upo (balaa), 4) hakuna umeme wala mawasiliano (balaa). Yote maisha.

At 3:15 AM, Blogger mloyi said...

Karibu tena, fanya uwezalo tuendelee kuwa pamoja maana naona Makene anasubiri umpashe hali ya huku ikoje na yeye afikiria uamuzi wake wakurudi au la.
Karibu tena.

At 6:06 AM, Blogger mwandani said...

ngaga fijo

At 8:19 AM, Blogger Rama Msangi said...

Kweli Mbeya kubwa siku hiuzi, tena tokea iitwe jiji nadhani. Mbeya hii hii au nyingine hatuonani mzee? Nipe ile namba maana niliharibikiwa na simu nilipoi-flash ikapoteza kumbukumbu zote. Nitumie kwa 0713 412176

At 7:45 AM, Blogger Alex Mwalyoyo said...

Umekuwa kimya mno Kaka, hebu tupe habari za hapo jijini Mbeya!

At 7:46 AM, Blogger Alex Mwalyoyo said...

This comment has been removed by a blog administrator.

Post a Comment

<< Home