Thursday, June 02, 2011

SOKO LA UHINDINI MBEYA LILIVYOPIGWA NYUNDO

Wazee wa jiji wameanza mpango wao wa kujenga soko la kisasa lilipokuwa soko la Uhindini liloungua miezi michache iliyopita. Kuanzia juzi nyundo mtindo mmoja kwa ajili ya ujenzi huo unaoongelewa na wengi kuwa utakuwa babu kubwa. Hakika hauwezi kula muwa bila kukuta fundo. Soko tulilizoea lakini wazee wa mji wamelizoea zaidi na sasa tunatarajia soko jipya.Wazee wa kazi kaziniMkabala na Tanesco, mitaa ya wakina-ChapaulingePicha kutokea NMB Mbalizi RoadUpande wa Lupa Way mkabala na Airtel na tiGOGROUND ZERO

Labels:

3 Comments:

At 6:02 PM, Blogger Goodman Manyanya Phiri said...

Mimi nimependa zaidi hiyo GROUND ZERO (tena juu ya kichwa cha Obama, aisee!)


ANYWAY, siku nitakapokuja tena TZ lazima nifike Mbeya. Naona vile kama THAT IS WHERE IT IS HAPPENING!!!


Au vipi?

 
At 12:40 AM, Blogger John Mwaipopo said...

ndugu goodman phiri tunakukaribisha sana mbeya. hali ya hewa ni baridi ya wastani sio kama joto la dar es salaam.

na mimi nataka nitembelee eastern cape miezi si mingi.

 
At 4:06 PM, Blogger Goodman Manyanya Phiri said...

@Mwaipopo

Nawe karibu sana, ila kama safari yako (Eastern Cape) ni kabla ya mwezi Agasti, kuwa tayari kukutana sio tu na baridi, bali hata barafu hapa bondeni. Lakini patakufaa sana wewe kwa rangi yako hiyo nyeupe nyeupe sio kama mimi cheusi (LOL!)

 

Post a Comment

<< Home