Wednesday, August 18, 2010

MWAKA HUU HAPATOSHI HAITI NA MBEYA



Huyu ni Wyclef Jean, mwanamuziki wa muziki wa kuruka-ruka (hip hop) ya ki-Marekani. Anagombea urais wa kisiwa cha Haiti. Kabla hajadhani kuwa atatamani kukiongoza kisiwa hicho kama rais alikuwa na ndoto ya endapo angekua rais wa Marekani. Kwenye ghani zake aliimba:

"If I was president,

I'd get elected on Friday,

Assassinated on Saturday,

And buried on Sunday,

I'd be back at work on Monday."




Na huyu ni Joseph Mbilinyi, mwanamuziki wa muziki wa kuruka-ruka (hip hop)wa ki-Tanzania. Mwaka huu anawania ubunge kwa tiketi ya CHADEMA jimbo la Mbeya mjini. Ghani zake zimekuwa zikichukuliwa ni za kimapinduzi na kutetea wanyonge. Sehemu ya ghani hizo iko katika wimbo Hali Halisi. (Nimepata tafsiri yake ya kiingereza na naiweka hivyo hivyo kwa kuchelea kuitafsiri katika kiswahili ambacho hakuimba yeye):

"Everyday is us against the police and the police against us

The judge at the court is waiting for us

The prison officer is waiting for us"

Labels:

1 Comments:

At 11:33 PM, Blogger Maisara Wastara said...

Ama kweli kaka patakuwa hapatoshi....

 

Post a Comment

<< Home