Tuesday, July 20, 2010

MAPENZI HOSPITALI YA VICHAA

Watu huonyesha upendo kwa njia mbalimbali. Sio lazima wakuonyeshe upendo kwa namna uzitakazo wewe. Sikiliza hii.

Omari na Edna walikuwa wamelazwa hospitali ya vichaa. Siku moja walipokuwa wakipita kando ya bwawa la kuogelea la hospitalini hapo, Omari akachumpia ndani ya bwawa la kuogelea upande wenye kina kirefu. Akapiga mbizi mpaka chini kabisa na akabakia huko. Edna kwa haraka akapiga mbizi kwenda kumuokoa Omari. Akafanikiwa kumuopoa kutoka katika kina cha bwawa.

Muuguzi mkuu aliposikia kitendo cha kishujaa cha Edna, maramoja akaagiza Edna aruhusiwe kutoka hospitalini kwa kuwa alimuona kuwa sasa amepona akili. Alipokwenda kumpasha habari akamwambia, "Edna, nina habari njema na mbaya kwako. Habari njema ni kwamba utaruhusiwa kurudi nyumbani kwa kuwa uliweza kuamua kwa usahihi katika janga kwa kuchumpa kwenye bwawa la kuogelea na kuokoa maisha ya mgonjwa mwingine. Nimejiridhisha kuwa kitendo chako kinaonyesha kuwa una akili njema sasa.



Habari mbaya ni kuwa Omari, yule mgonjwa uliyemuokoa, amejinyonga bafuni na taulo baada ya kuokolewa na wewe. Pole sana lakini amekufa." Edna akajibu, "Hakujinyonga, mimi nilimning’iniza pale akauke. Lini nitaruhusiwe kwenda nyumbani?"

Labels:

5 Comments:

At 6:56 AM, Blogger Fadhy Mtanga said...

Ha ha ha ha haaaaaaaaaa.....kaka John hi hi hihi hiiiiiiiiiiii.........ooooooossh... Nimecheka vibaya mno kaka.

Mi nadhani Edna aongezewe muda wa kukaa hospitali.

 
At 9:21 AM, Blogger Yasinta Ngonyani said...

Nilipoanza kusoma nikaona ndoto na nilipofikia mwisho nikasema uwiiiiii wala Edna asiruhusiwe na akiruhusiwa atawaning´iniza wengiiii-

 
At 1:19 PM, Blogger Mija Shija Sayi said...

Eeeeeh bwana eeh!

 
At 4:02 AM, Blogger o'Wambura Ng'wanambiti! said...

Mi naomba aruhusiwe apangiwe dispensari/hospitali wanayotibiwa wakubwa wale wanaowkwenda nje saaana!

 
At 8:24 AM, Blogger chib said...

Yaani kazi yote ni kiduara.

 

Post a Comment

<< Home