Tuesday, August 10, 2010

KISWAHILI CHA MTAANI

Katika kila lugha kuna lugha ya matumizi makuu na ile ya matumizi ya mitaahi. Maneno ya mitaani huja, hutumika na mengine huondoka. Mengine hurasimishwa na kutumiaka katika matumizi rasmi. Hii hutokana na kutokuwepo kwa neno lifaalo kabla ya hilo la matumizi ya kimtaa-mtaa. Mfano, katika miaka ya 80 kuliibuka aina ya uhalifu wa kudanganya watu. "Wasela" wakauita wizi huu "utapeli". Somo likomee hapa.


Kinyago ya kimakonde

Kiswahili cha mtaaani cha siku hizi kina maneno haya hapa chini. Nachelea kujiaminisha kuwa naelewa maana zake vema. Naomba mwenye kuyaelewa anisaidie. Profesa Matondo nadhani anayajua haya.

kuuza nyago (inatokana na 'kinyago')
mpago mzima
Kusepa
Ku-show love

Labels: ,

3 Comments:

At 4:36 AM, Blogger Yasinta Ngonyani said...

Kaka John ahsante kwa somo zuri la kiswahili si unajua tena ukikaa huku miezi sita ukirudi kila kitu kimebadilika hata kiswahili unabaki kama mgeni kwelikweli.

 
At 4:24 PM, Blogger Simon Kitururu said...

Ilo la ``Ku- show Love ´´uswahili wake naona umekonda.:-)

 
At 11:35 PM, Blogger Maisara Wastara said...

Na kuchakachua je?

 

Post a Comment

<< Home