BRING HIM (MANDELA) BACK HOME
Mwaka 1988 wakati familia yetu ikishi Morogoro wazungu fulani wakimbatana na wakimbizi wa Afrika ya Kusini waliokuwa wakiishi Mazimbu walimpa baba yangu kanda ikiwa na wimbo 'Bring Him Back'. Wimbo ulikuwa na maudhui ya kutaka Nelson Mandela aachiliwe kutoka kifungoni. Hapa chini ni Vidio Yake. Umeimbwa na aliyewahi kuwa mume wa marehemu Miriam Makeba, Hugh Masekela.
Hivi majuzi babu Mandela ametimiza umri ya miaka 92. Nampongeza kwa kumpigia video yii. Kibwagizo kinaenda hivi:
Bring back Nelson Mandela, Bring him back home to Soweto
I want to see him walking down the streets of South Afrika
Bring back Nelson Mandela, Bring him back home to Soweto
I want to see him walking hand in hand with Winnie Mandela
Nelson Mandela na Walter Sisulu wakiwa gerezani
Sauti ya Vuvuzela (Baragumu) inamtakia miaka mingi mbeleni.
Labels: freedom, hugh masekela, mandela
6 Comments:
ni kumbukumbu nzuri kwa kweli. Na ni vema sana kutunza kumbukumba kama hizi ili tuweze kuwaonyesha na vijukuu .
Nami pia namtakia afya njema.
Swali kaka. Hivi ni sahihi kwa mtu wa umri wa Mandela kusema twamtakia maisha marefu? Ni swali tu.
Pia sikujua hiki kijiwe kimekuwa vuvuzela sasa. hongera sana
fadhy nadhani mambo ya lini mtu atakoma kuishi duniani ni ya mungu mwenyewe.
This comment has been removed by the author.
This comment has been removed by the author.
Sauti ya Vuvuzela!? Haya. Nami pia namtakia maisha marefu mzee Madiba.
Post a Comment
<< Home