Friday, July 30, 2010

SHILINGI YAUA- SIMBA WA NYIKA



Tuselebuke kizamani-zamani

Kwa ijumaa hii si vibaya tukawasikiliza Simba wa Nyika katika Shilingi Yaua. Gonga hii link hapa chini.

http://www.ntwiga.net/linked_to_audio/Simba_Wanyika-Shilingi_maua_tena_maua

Kuna mtu anaweza nitajia majina yote ama baashi ya kundi la Simba wa Nyika

Labels:

8 Comments:

At 6:50 AM, Blogger Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Simba wa Nyika - mojawapo ya bendi bora kabisa kutoka Afrika Mashariki.

Umenikumbusha mbali sana. Kijijini kwetu kulikuwa na jamaa mmoja ambaye alikuwa na redio kubwa yenye uwezo wa kucheza kaseti na nyimbo hizi zilikuwa mashuhuri sana. Kila siku jioni ilikuwa lazima twende nyumbani kwake kusikiliza muziki na nyimbo za Kisukuma.

Huyu jamaa alikuwa na baiskeli mpya iliyokuwa imeandikwa KAMINOMINO MPENDA WASICHANA. ULIZA SABABU YAKE. Bahati mbaya baadaye UKIMWI ulipokuja ndiye alikuwa mtu wa kwanza kwanza kuondoka pale kijijini pamoja na wake zake watano! Huzuni kweli.

Ni kama juzi tu kumbe ni zaidi ya miaka karibu 30 sasa. Maisha!

 
At 8:12 AM, Blogger Yasinta Ngonyani said...

Kaka John kwa kweli ijumaa ya leo ni kweli kuselebuka maana nimejikuta naselebuka na kujiona nipo mdogo tena. Maana hizi nyimbo nimezisikia tangu nilipoingia katika dunia hii marehemu mama yangu alikuwa anaziimba utazani yeye ndio redio. Ahsante kwa kumbukumbu hii.

 
At 12:02 AM, Blogger nyahbingi worrior. said...

kweli,tukumbuke za zamani.

 
At 2:02 AM, Blogger John Mwaipopo said...

hadithi ya kuhuzunisha ya mwalimu matondo.

yasinta hukurithi kipaji cha kuimba?

nyahbingi ya kale dhahabu

wanasema muziki ni kitu pekee kinachoweza kurudisha hisia na kumbukumbu kwa haraka, kikifuatiwa na picha.

nimepekua mtandaoni na kupata majina ya waanzilishi wa hii bendi ambao walikuwa watanzania wa tanga ndugu Wilson Kinyonga na George Kinyonga

wanamuziki wengine?

 
At 4:42 AM, Blogger Simon Kitururu said...

ASante Mkuu kwa hii kitu ! Maana imenisuza roho kimswano!:-)

 
At 4:42 AM, Blogger Simon Kitururu said...

ASante Mkuu kwa hii kitu ! Maana imenisuza roho kimswano!:-)

 
At 11:56 AM, Blogger chib said...

Subi atakuwa na data base, wasiliana naye atakupa :-)

 
At 2:14 AM, Blogger emuthree said...

Enzi hizo bwana, hakuna kutoka jasho, mmmh kila kitu na wakati wake

 

Post a Comment

<< Home