Saturday, December 16, 2006

Ajali Ya Ndege Mbeya

Leo asubuhi imetokea ajali ya ndege hapa mjini mbeya eneo la uwanja wa ndege wakati ikianza kupaa kuelekea Dar es Salaam. Waliokuwamo ndegeni ni Naibu Waziri Juma Akukweti, rubani, mwandishi habari wa kike na mtu mwingine. Inasemekana mwandishi amefariki dunia papohapo. Waziri, rubani, mtu mwingine wamejeruhuiwa.

Nyepesinyepesi za hapa Mbeya zinatonya kuwa kuna mkono wa mtu kwani Waziri alikuja jana kujua hali halisi ya moto ulioteketeza soko la Mwanjelwa. Wanazi hao wanadai kuwa mkutano baina ya waziri na wahanga (wafanyabiashara) wa Mwanjelwa haukutoa majibu ambayo yaliwafurahisha wahanga. Wahanga wanataka kuruhusiwa kujenga upya ili waendeleze biashara zao wakati serikali imeamua kuwa huo ndio mwisho wa soko la Mwajelwa.