Wednesday, June 08, 2011

RENATHA BENEDICTO UNATAFUTWA HUKU...!!


Mubelwa Bandio katika pozi

Ndugu. Kwa mara nyingine nawakilisha ombi la kunisaidia kutangaza (wakati wowote upatapo nafasi) kuhusu Dada mdogo RENATHA BENEDICTO ambaye tumepoteana kwa takriban miaka 12 sasa.

Renatha alikuwa mwanafunzi wa shule ya Sekondari Kibasila jijini Dar kati ya mwaka 1998 - 2001 na baada ya hapo alienda Songea TTC kujiunga na masomo ya ualimu. Pia alikuwa kati ya wahanga wa ajali mbaya ya Tawfiq iliyotokea tarehe kama ya leo mwaka 1999 ambapo alikuwa msaada mkubwa saana kuokoa maisha yangu. (Maelezo kamili yako HAPA KWA MUBELWA MWENYEWE)

Niliwasiliana naye kwa miaka miwili iliyofuata mpaka alipoenda chuoni Songea nami nikaondoka nchini mwaka 2003 na kwa miaka mingi sasa nimekuwa nikijitahidi saana kumtafuta bila mafanikio. Naomba kama anaweza kusoma ama kuna anayesoma na kumfahamu anisaidie kuwasiliana naye.
Email yangu ni changamoto@gmail.com

NATANGULIZA SHUKRANI

Labels:

5 Comments:

At 7:15 AM, Blogger Yasinta Ngonyani said...

Jamani ajuaye Dada Renatha aliko twaomba awasiliano na kaka Mubelwa anamtafuta...nina ushauri au jaribio labda tupeleke tangazo redio Maria....

 
At 7:22 AM, Blogger John Mwaipopo said...

kwa kweli nakubaliana na dada yasinta ngonyani. ukisoma maandiko yake ndugu Mubelwa Bandio unaona kabisa anasema kutoka katika sehumu tulivu kabisa ya moyo wake wa kitanzania/kibukoba.

Pia Radio Free Afrika wana kipindi cha Search Line. Sijui kiko lini ngoja nitafiti. I can feel how Musee ya Changamoto is desperately looking for this lady.

 
At 11:21 AM, Blogger Goodman Manyanya Phiri said...

Renatha ni malaika yule! Katenda wema na kuondoka zake. Vilevile shukrani haidai kwa mtu yoyote.


Tunaweza Nduguzanguni kuwatafuta wale waliotufanyia mema ili tuwapongeze au tuwashukuru. Ukweli lakini ni kwamba kwao malaika hatudaiwi lolote kwa msaada wao; bali tunadaiwa kutoa shukrani zetu kwa Mungu hapo tulipo kwa wakati wa sasa kwa kusaidia nasi viumbe Vyake viliokuwa karibu nasi.

 
At 1:39 PM, Blogger Mzee wa Changamoto said...

Thanx all.
Ninazidi kupata matumaini kwamba nitampata punde.
M'BARIKIWE NYOTE

 
At 3:05 PM, Blogger SIMON KITURURU said...

Mubelwa Bandio kwa mtazamo wangu ana roho nzuri kweli yani !


Ila naye kama siye ,...
... labda usiwaulize nzi WALIOWAHIKUWEPO ukutani WAKATI anafanya kuwa alikuwa anafanya nini- lakini kiroho nzuri tu kwenye vyumba fulani!

Labda unaweza kustukia huwa nakaba mtu hata kama nia ni kumfikishia huyo mtu heri ya utamu.

Nawaza tu kwa SAUTI!:-(

 

Post a Comment

<< Home