Friday, February 02, 2007

Sauti Ya Baragumu Yatimiza Mwaka Mmoja

Ni furaha ilioje leo kukumbuka kuwa mwaka mmoja uliopita blogu hii ndipo ilipozaliwa hapa. Na ilianza kimzahamzaha kama hivi. Kumbe blogu, pamoja na mambo mengine, ni teknolojia nzuri kutunza kumbukumbu. Binafsi nemecheeka sana kukumbuka enzi hizo!

Ingawahe ilianza kwa kishindo baadaye ilififia kidogo kutokana na mimi kurejea kwetu hapa. Si mnajua mambo ya mitandao huku. Hata hivyo azma yake ya kupashana habari bado mbichi. Pengine sasa nimeanza kutulia na kujipanga upya. "Epi bethidei" Baragumu.
Pichani nipo maabara ya kompyuta makao makuu ya chuo ninachofundisha Tanzania Institute of Accountancy, Dar es Salaam.

9 Comments:

At 3:01 AM, Blogger mwandani said...

Nimetafuta wimbo wa hepi bethdei wa kiswahili nimeshindwa. Nasema kwa kizungu: hepi bethdei Baragumu!

 
At 6:06 PM, Blogger MTANZANIA. said...

Hongera kwa kutimiza mwaka kaka. Usisite kunitembelea maana mie nina takribani mwezi moja. Karibu sana.

 
At 5:11 PM, Blogger Alex Mwalyoyo said...

Hongera sana kwa kutimiza mwaka mmoja. Kwa kumbukumbu zangu ni kwamba safari yako ya kublogu ilianza miaka ya nyuma kidogo,siyo mwaka jana, nakumbuka kuwa mnamo mwaka 1997 tukiwa mkoani Iringa tunasoma ulikuwa unablogu katika *tovuti* (gazeti) ya SAZIA kama mhariri mkuu. Moja ya kazi zako (hasa kile kikaragosi cha basi lililobeba wanafunzi) ilileta matatizo na watawala wa mahali pale na nadhani ndio hapo ukapata na uzoefu wa namna vyombo vya dola vilivyo kinyume na habari mbadala. Mkasa kama wako pia ulimkumba na mchora vikaragosi Aloyce Kitule mwaka uliofuatia,(nadhani unamkumbuka vizuri) kwa kuwa aligusa mahali pabaya pa dola ya pale kwa wakati ule. Hata hivyo mkasa huo haukukukatisha tamaa nadhani ndio sababu hadi leo umeendelea kusimama na unablogu hapa tovutini. Tofauti na wakati ule, leo unablogu ukiwa huru zaidi na kazi zako zinasomwa na umati mkubwa zaidi kwa sababu ya hii Teknohama. Mi mwenyewe nilianzisha blogu yangu kutokana na mchango wa mawazo yako mwaka jana, mara baada ya wewe kunipa anuani yako ukiwa nje ya Tanzania. Naomba uendelee kutupasha habari zaidi na zaidi bila kukata tamaa.

 
At 6:00 AM, Blogger mloyi said...

Baragumu imekuwa sasa, kama imeshinda mengi katika kipindi kilichopita, tunaamini sasa tutakuwa nayo kwa kipindi kirefu zaidi.

 
At 12:17 PM, Blogger MTANZANIA. said...

Baragumu!
Baada ya mwaka moja mbona kimya kulikoni tena!

 
At 10:52 PM, Blogger Simon Kitururu said...

Ingawa nimechelewa!Hongera Sauti ya Baragumu!

 
At 9:58 AM, Blogger Jeff Msangi said...

Hongera Sauti ya Baragumu

 
At 12:19 PM, Blogger MICHUZI BLOG said...

hongera sana baragumu kwa kutimiza mwaka. kwa kweli nafarijika kuona umeanza kutroti tena baada ya ukimya mrefu (toka ajali ya ndege, lol!) umeanza kupuliza bnaragumu.

 
At 4:02 AM, Blogger Christian Bwaya said...

Hongera sana Baragumu. Mwaka moja si mchezo!

 

Post a Comment

<< Home