Wednesday, June 29, 2011

VYUNGU VYA MAUA
Nilikwisha kurudi jijini Mbeya tangu juma lililopita. Sijaweza kublogu kuwajulisha yatokanayo na safari yangu kwa sababu ambayo wote mnaweza KUBASHIRI. Naam wote mmepatia.Leo imetokea bahati tu 'upo'. Safari yangu ilikuwa na breakdown nyingi, moja kati ya hizo ilitufikisha katika kijiji cha Rungemba, katikati ya Ifunda na Mafinga. Hapo kuna wafinyanzi wabunifu kama picha zinavyojielekeza.


Vyungu vya maua. Kwa mbali basi letu likikarabariwa.



Kwa karibu



'Buti'kwa Mbele



'Buti' kwa nyuma

Chungu kimoja huuzwa kwa 15, 000/-, kwa watalii inafika hata 25,000/-

2 Comments:

At 2:13 AM, Blogger Subi Nukta said...

John, siku ukifanikiwa kufika Iringa, ulizia kituo cha Faraja cha Fr. Sordella, kipo katika kijiji cha Mgongo (mbele tu ya Kihesa, kabla ya kufika Nduli), wana VTC vijana pale walitengeneza hivi viatu "ndula" halafu wakapanda maua, basi vinapendeza kweli urembo. Nilipiga picha, siku nikipata muda nitaiweka kwenye blogu uone.
Nimefurahi kuona wazo hili kumbe limezaliwa na kuendea kwingine pia.

 
At 5:24 AM, Blogger John Mwaipopo said...

hakika subi hizi ndula bomba sana kwa maua. nilitamani nidake moja isipokuwa aina ya usafiri ilinifanya 'nisiwaungushe' masela wale.

 

Post a Comment

<< Home