Thursday, December 30, 2010

SHUKURANI 2010


Mapozi Kijiweni

Napenda kujichukulia nafasi hii ya masaa haya machache kabla ya kuisha kwa mwaka 2010 kuwashukuru watu woote ndani ya blogu na nje ya blogu kwa yale mema yote waliyonitendea. Nashukuru kwa wao kufikiri nilistahili kutendewa mambo mema.


Kazi na Muziki

Nawatakieni wote wakati mzuri tukiusubiri mwaka 2011 kwa amani na upendo. Pia nawatakieni mwaka wa mafanikio na mabadiko chanya katika maisha yenu. Basi tukiusubiri mwaka ujao si vibaya tukajiliwaza kwa kumsikiliza na kumtazama SAM WA UKWELI katika songi lake hili SINA RAHA ambalo kwa mtazamo wa wengi limekimbiza sana miezi hii ya mwisho wa mwaka huu.



Kuna mistari fulani ya songi hili huwa siipati vyema utadhani kamimba kiyunani vile

alamsiki binuur

Labels:

10 Comments:

At 3:09 AM, Blogger Yasinta Ngonyani said...

Kaka John nakubaliana kweli una pozi. Haya ngoja tusubiri kuuvuka mwaka huu 2010 kwa amani. BASI NGOJA NIKUTAKIE KHERI YA MWAKA UJAO 2011!!

 
At 6:36 AM, Blogger Simon Kitururu said...

Kila la kheri Mkuu!

 
At 4:42 PM, Blogger Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Kila la heri Mwalimu. Mapya na mazuri zaidi kwa mwaka huu. Pamoja daima!!!

 
At 1:46 PM, Blogger Christian Bwaya said...

Nikutakie mema yote kwa mwaka unaofuata!

 
At 4:47 PM, Blogger Mija Shija Sayi said...

Heri ya Mwaka mpya...

 
At 8:46 PM, Blogger emuthree said...

Mwaka huo umeshaanza kupiga makasia, twasubiri baragumu lilie na mambo mapya, kwani wahenga husema `akili ni nywele kila mtu ana zake...kila la heri mkuu

 
At 12:07 AM, Blogger Alex Mwalyoyo said...

Tumekupata kaka.
Heri ya mwaka mpya na kwako!

 
At 2:39 PM, Blogger Yasinta Ngonyani said...

Kaka Jonh Upo?????

 
At 6:53 PM, Blogger Mzee wa Changamoto said...

Duh!!

 
At 8:22 AM, Blogger chib said...

Hao wanafunzi watafaulu kweli!Kila la heri

 

Post a Comment

<< Home